Wednesday, January 20, 2021

CHAPECOENSE KUPEWA TAJI LA COPA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

CHAPECO, Brazil


CHAPECOENSE watavikwa ubingwa Copa Sudamericana kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL), Ivan Tozzo.

Kikosi hicho cha Brazil kilichopoteza mastaa wake  19 kwenye ajali ya ndege iliyotokea Jumanne ya wiki iliyopita nchini Colombia na watu 71 kupoteza maisha yao.

Timu hiyo kilichopewa jina la utani la ‘Leicester City ya Brazil’, ilikuwa ikienda kucheza fainali ya kwanza ya Copa Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional kabla ya kupata ajali hiyo mjini Medellin, Colombia.

Kufuatia ajali hiyo, mabingwa wa Colombia, Atletico Nacional waliliomba Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) kuwatangaza Chapecoense kuwa mabingwa kama sehemu ya heshima.

Hivyo ombi lao linaonekana kama linaweza kuwa kweli, baada ya rais wa muda wa shirikisho hilo, Tozzo kusema kwamba taji la Copa Sudamericana litakabidhiwa kwa kikosi hicho cha Brazil.

Taarifa hiyo imesema: “CONMEBOL imeweka wazi kwamba watawavika Chapecoense ubingwa huo wa Copa Sudamericana.”

Dunia ya wapenda soka wamekuwa wakiomboleza wiki nzima, vilabu mbalimbali duniani vikikumbuka vifo vya wachezaji hao kwa kusimama kimya dakika moja katika kila mechi, huku wengine wakionyesha fulana zao za ndani wakati wa kushangilia mabao wanayofunga.

Tayari wachezaji wakongwe kama Ronaldinho na Juan Roman Riquelme wametoa ofa ya kuicheza klabu hiyo, ili kuisaidia kuundwa upya kwa kikosi hicho.

Wakati klabu za Brazil zikitoa wachezaji kwa mkopo bure kujenga kikosi hicho, pia kikosi hicho kinadaiwa hakitashushwa daraja kwa miaka mitatu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -