Tuesday, November 24, 2020

CHEKA ATAFUTA MACHUNGU KWA DULA MBABE?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

BAADA ya kupoteza pambano lake nchini India bondia, Francis Cheka, amerejea jijini Dar es Salaam leo tayari kujiandaa na pambano lake dhidi ya bondia, Abdallah Pazi ‘Dula Mbabe’, litakalofanyika  Desemba 25 kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba.

Cheka amerejea ikiwa ni siku chache baada ya kupigwa kwa (TKO) na bondia Vijender Singh, katika pambano lililofanyika kwenye Uwanja wa Thyagaraj mjini New Delhi, India.

Baada ya kipigo hicho, Cheka atapanda tena ulingoni Desemba 25, mwaka huu kuzipiga na Dula Mbabe, katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya kupigwa na Singh, mara ya mwisho Cheka alipanda ulingoni Februari 27, mwaka huu alimpomshinda kwa pointi, Geard Ajetovic wa Serbia viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam na kutwaa taji la WBF Intercontinental uzito wa Super Middle.

Tayari mabondia hao wameshaingia mafichoni kujiwinda na pambano hilo ambalo pia ni sehemu ya shamrashamra ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ambazo hufanyika mwishoni mwa mwaka.

Promota wa pambano hilo, Kaike Siraju, aliliambia gazeti hili kuwa maandalizi ya kuelekea pambano hilo yanaendelea vizuri na mabondia hao tayari wapo kambini hapa jijini na huko Morogoro kwa lengo la kujiweka fiti.

“Ni jambo lisilofichika, Cheka na Dula Mbabe ndio mabondia bora na wanaofanya vizuri kwa sasa hapa nchini, hivyo tumeona ni vyema tuitumie Sikukuu ya Krismasi kama sehemu ya kumaliza ubishi kati ya hawa mabondia.

Cheka amekuwa akiendelea kujifua mkoani Morogoro, wakati Dula Mbabe amejichimbia jijini Dar es Salaam,” alisema Siraju.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -