Friday, December 4, 2020

CHEKA UKIPOTEZA KWA DULLA MBABE, TANGAZA KUSTAAFU NDONDI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA WINFRIDA MTOI

HIVI karibuni bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka, alipoteza pambano kwa kupigwa ‘Technical Knockout (TKO),’ raundi ya tatu na bondia wa India, Vijender Singh, lililofanyika Uwanja wa Thyagaraj, mjini New Delhi, nchini humo.

Pambano hilo lilikuwa la ubingwa wa WBO, Asia Pacific katika uzito wa Supper Middle na aliyekuwa anashikilia ubingwa huo ni mpinzani wake, hivyo ameshindwa kumnyang’anya mkanda huo.

Hata hivyo, baada ya kupoteza mchezo huo, Cheka alitoa visingizio vingi vilivyomfanya ashindwe katika pambano hilo, ikiwamo kudai kufanyiwa hujuma kutokana na begi lake alilokuwa ameweka kikinga meno chake kupitilizwa na ndege kwenda Marekani.

Kutokana na hilo, ikamfanya kutumia kifaa ambacho hakikuwa saizi yake, ndiyo sababu kubwa ya kushindwa kuendelea na pambano na mpinzani wake kupewa ushindi kwa kuwa kifaa hicho hakikuweza kushika vizuri kwenye meno.

Je, sababu hizo zinatosha kwa Cheka kuwaaminisha Watanzania, hasa wapenda ngumi kwamba anachokisema ni kweli, ukizingatia imekuwa ni kawaida kwa wanamichezo wengi wa Tanzania wanaposhindwa kufanya vizuri nje ya nchi hurudi na visingizio lukuki.

Sawa kuna hujuma nyingi hufanywa kwa wanamichezo, hasa wanapokuwa ugenini, lakini bado kuna kasoro zinazojitokeza katika maandalizi pindi wanamichezo wengi wanapokwenda nje ya nchi kushiriki mashindano zinazosababisha kushindwa.

Malalamiko ya Cheka kwa pambano la juzi yanaweza yakawa ni kweli, lakini je, kiwango chake cha sasa katika masumbwi kikoje na angeweza kustahimili raundi 10 za mchezo ule hata kama angekuwa na vifaa vyote?

Ukiachana na kiwango chake siku hizi, hata alivyokuwa kwenye chati za juu, ilikuwa ngumu kwa Cheka kushinda mapambano ya nje na mara nyingi visingizio ndiyo hivyo hivyo, hujuma. Ukweli ni kwamba, Cheka hata alivyokuwa kwenye kiwango kizuri bado mapambano ya nje yalikuwa yanampa shida.

Ninakubali Cheka ni bondia mzuri aliyejipatia heshima kubwa, kutokana na kazi yake, ila anachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuweka bayana juu ya kiwango chake kilipofikia ili kuweza kutafutiwa mapambano yanayoendana naye au ikishindikana kabisa ni kustaafu kabisa.

Mapambano yake ya miaka ya hivi karibuni yamedhihirisha hayuko kwenye kiwango chake kile cha kuitwa SMG, nikiwa na maana kiwango chake kimeshuka tofauti na awali.

Mara ya mwisho Cheka kucheza pambano la kimataifa ilikuwa Februari mwaka huu, alipopanda ulingoni kupigana na Geard Ajetovic wa Serbia, katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam na kutwaa taji la WBF na walioshuhudia mchezo huo wanaweza kujua wapi kiwango cha bondia huyo kilipofikia kwa sasa.

Licha ya ushindi alioupata wa pointi, bado yaliibuka malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa mchezo wa ngumi  nchini kutokana na kiwango cha chini alichokionyesha na kuonekana kuwa hakustahili kutwaa ubingwa huo.

Tukiachana na hayo, Desemba 25, mwaka huu, Cheka anatarajia kupanda tena ulingoni kupigana na bondia anayekuja juu kwenye masumbwi, Abdallah Pazi, maarufu Dulla Mbabe, katika pambano lisilokuwa la ubingwa kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mabondia hawa kukutana, wakiwa wote wametoka kupoteza michezo yao mwezi huu. Kutokana na historia ya Cheka katika tasnia hii ya masumbwi, endapo atashindwa katika pambano hili, atatakiwa kutangaza hadharani kuwa anaachana na mchezo huu.

Nasema hivyo kwa sababu baada ya kufariki kwa Thomas Mashali, mpinzani pekee aliyebaki kwa Cheka ni Dulla Mbabe, hivyo akifanikiwa kuibuka na ushindi atakuwa amejiweka juu ya Cheka.

Hivyo ili Cheka ajiweke salama na kuendelea kulitunza jina lake, anatakiwa kuachana na mchezo huo kama alivyofanya Rashid Matumla, baada ya kuona mabondia wenzake wanamzidi kiwango.

Ni wazi kuwa, kwa kiwango alichokuwa nacho Dula Mbabe kwa sasa, Cheka atakuwa na kibarua kizito ili kuweza kuibuka na ushindi kwenye pambano hilo siku ya Jumapili.

Nina imani kuwa washauri na  watu wa karibu wa bondia huyo mkongwe nchini, watakuwa makini kufuatilia kile atakachokuwa anakifanya ulingoni na kulinganisha na michezo ya miaka ya nyuma, ikiwamo pambano alilopigwa na Mashali Morogoro ili kumwezesha kuja na uamuzi sahihi, endapo atapigwa siku ya Krismasi aachane na mchezo huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -