Wednesday, November 25, 2020

CHELSEA MSIJIVUNGE KWA LUKAKU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA OSCAR OSCAR

KATIKA umri wa miaka 23 ni wachezaji watatu tu ambao waliwahi kufunga mabao mengi ya ligi kuu nchini England kuliko kijana wa Kibelgiji, Romelu Lukaku. Akiwa na miaka 23, Wayne Rooney alifanikiwa kufunga mabao 86.

Michael Owen alifunga mabao 110 na Robbie Forler 106. Tofauti na hapo, utalitaja jina la Romelu Lukaku. Sioni sababu ya Chelsea kutomrejesha Lukaku nyumbani, Stamford Bridge. Kijana ameiva na anaonyesha utayari wa kupigania nafasi ndani ya Chelsea.

Ni kama Manchester United walivyomtazama Paul Pogba akiwa Juventus na kumrejesha nyumbani, Old Trafford. Ni kama Real Madrid walivyoamua kumrejesha nyumbani, Santiago Bernabeu kijana wao Alvaro Moratta. Ukiachilia mbali uwezo mkubwa wa Lukaku, umri pia bado unamruhusu. Bado ana mika 10 mbele ya kufunga mabao, bado ana kiu ya kushinda mataji.

Pamoja na kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea wanahitaji kuongeza nguvu kwenye idara ya ushambuliaji hususani kuelekea msimu ujao ambapo watakuwa wakirejea kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Chelsea imekuwa timu inayomtegemea zaidi Diego Costa kwenye ushambuliaji ambaye mpaka sasa amefunga mabao 18 tu kwenye michuano yote. Eden Hazard nae anaonekana kurejea kwenye makali yake na mapaka sasa amefunga mabao 11 kwenye michuano yote msimu huu.

Unapomtazama Lukaku, unagundua kwamba idadi ya mabao aliyopachika kwenye EPL pekee, imezidi yale ya Diego Costa. Hakuna haja ya Chelsea kwenda nje ya England kumsaka msaidizi wa Costa, Lukaku amekamilika kwa kila kitu.

Romeru Lukaku ameizoea Ligi ya England na anapajua vizuri darajani, ni muda wake wa kuja kufanya kazi. Tayari msimu huu ameshapachika mabao 19 ya EPL na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Klabu ya Everton kwenye EPL baada ya kufikisha mabao 62 ndani ya klabu hiyo.

Ni muda wa kuona mabao ya Lukaku hayapotei bure. Ni muda wa kushuhudia Lukaku akishinda mataji. Kama anaweza kupachika mabao 19 nyuma yake akichezeshwa na viungo kama Ross Barkley, Kelvin Mirallas itakuwaje akichezeshwa na watu kama Eden Hazard na Cesc Fabregas?

Hakuna haja ya kwenda Ujerumani wala Hispania kwa Chelsea kuongeza nguvu, Lukaku ni chaguo sahihi kwa sasa. Kuna washambuliaji wengi kwa sasa duniani lakini Real Madrid waliamua kumrekebisha kijana wao Alvaro Moratta na maisha yakasonga.

Pamoja na kuwa hajapata nafasi moja kwa moja kwenye kikosi cha Real Madrid, Moratta ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi msimu huu akitokea benchi kwenye La Liga.

Pamoja na kuwa viungo wako wengi, Manchester United walivunja benki na kumrejesha Paul Pogba ambaye kwa sasa ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi kwenye eneo la mpinzani kuliko kiungo mwingine yeyote ndani ya EPL.

Chelsea mnasubiri nini? Huu ni muda mwafaka wa kuvunja benki na kumrejesha Lukaku. Uzuri wa namba huwa hazidanganyi kwenye soka, namba za Lukaku pia hazidanganyi. Msimu wa 2012/2013 Chelsea walimpeleka kwa mkopo West Bromwich na akafanikiwa kumaliza msimu akiwa na mabao 17 ya EPL.

Msimu uliofuata, 2013/2014 alipelekwa kwa mkopo ndani ya Everton na kumaliza msimu akiwa na mabao 15. Msimu uliofuata alifunga mabao 10 na msimu uliopita akawashawishi Everton wamnunue moja kwa moja baada ya kupachika kambani mabao 18.

Leo hii msimu haujaisha na ameshafunga mabao 19, Chelsea wanajivunga kwa lipi? Ni muda wa kumrejesha Lukaku ili aendeleze mpera mpera akiwa na fundi mwenziye wa Kibelgiji, Hazard.

Umri bado unaruhusu, anaifahamu vema Ligi ya England na Stamford Bridge, namwona Lukaku akitakata chini ya Antonio Conte. Namwona Lukaku akishinda mataji, namwona Lukaku akijitengenezea Ufalme darajani. Muda wa kumrejesha kijana nyumbani umewadia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -