Saturday, October 31, 2020

CHELSEA YAMPA RAHA SARRI,  ATANGAZA KUACHANA NA ‘FEGI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

LONDON, England

 


 

KOCHA wa Chelsea, Maurizio Sarri ,amesema kwamba anatarajia msimu huu timu hiyo haitampa msono wa mawazo na akasema kuwa hali hiyo itamfanya aachane na kuvuta sigara.

Kocha huyo wa  Blues anaonekana kuwa na mwanzo mzuri kwa kupata ushindi mara mbili katika michuano ya Ligi Kuu England na ushindi wa mabao  3-2 alioupata dhidi ya  Arsenal  unaonekna kuwa mzuri zaidi kuliko ambao aliupata katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya  Huddersfield Town.

Chelsea ilifanikiwa kupata mabao mawili ya kuongoza  kipindi cha kwanza, lakini wakafanikiwa kuondoka na pointi tatu kwa baoa lililofungwa dakika za mwisho na staa wao  Marcos Alonso.

Ushindi huu mara mbili ambao ameupata katika michezo miwili unaonekana kumfanya  Sarri  akiwa roho kwatu na kutokana na kuwapo kwa sheria ya kuzuia uvutaji sigara katika viwanja vya  ichezo nchini England itamfanya kocha huyo apate nafasi ya kuachana nazo.

Akizungumza juzi, kocha huyp wa zamani wa  Napoli alisema kuwa vita hiyo ya kuacha sigara ndiyo atakayobaki nayo, baada ya timu yake kuonesha mwelekeo wa kufanya vizuri.

“Nahitaji muda wa nusu saa ama kipindi cha kwanza hadi  hadi mwisho sitavuta sigara,” kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari.

“Nitaacha kwa muda wa mwaka mmoja ama miwili na baada ya hapo nitaanza kuvuta. Ilikuwa ndani ya dakika 15 ambapo tulikuwa taabani, tulishindwa kupiga pasi, tulishindwa kujiami kwa ujumla tulikuwa kwenye hali mbali,”aliongeza kocha huyo.

“Ila nadhani kipindi cha pili tulifanya vizuri na kurejea kwenye ubora wetu,”aliongeza zaidi kocha huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -