Sunday, October 25, 2020

CHELSEA YAPATA 10 KWA 10 WAKATI IBRA AKIIOKOA MANCHESTER UNITED

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England

BAO la Cesc Fabregas liliisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland juzi Jumatano usiku, ukiwa ni ushindi wao wa 10 katika mechi zao 10 mfululizo wakati kocha Antonio Conte akijikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa pengo la pointi sita zaidi ya Liverpool na Arsenal.

Fabregas, ambaye alichukua nafasi ya Nemanja Matic, aliunganisha mpira wa Willian dakika ya 40 na kuisaidia Chelsea kuweka rekodi ya kushinda mechi nyingi za ligi mfululizo tangu mwaka 2005-06.

Pamoja na ushindi wa klabu hiyo ya Blues, nao Liverpool, Manchester City na Tottenham Hotspur walikusanya pointi tatu kwenye mechi zao, huku mshambuliaji, Zlatan Ibrahimovic,  akifunga bao dakika ya 88 na kuisaidia Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace.

Chelsea, walimkosa Eden Hazard kutokana na kuwa majeruhi, lakini walifanikiwa kushinda mechi yao ya 10 tangu walipochapwa mabao 3-0 na Arsenal, Septemba 24 mwaka huu, huku wakicheza mechi nane kati ya hizo 10 bila ya kuruhusu nyavu zao kuguswa.

Kikosi hicho cha Conte kiko kileleni kikiwa na pointi 40 sita zaidi ya Liverpool, ambao wameiondoa Arsenal nafasi ya pili baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Middlesbrough, ingawa wote wana pointi sawa 34.

Baada ya Liverpool kuchapwa mabao 4-3 dhidi ya Bournemouth na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya West Ham, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, alimpumzisha mlinda mlango, Lorus Karius na kumwanzisha Simon Mignolet na Adam Lallana kufunga mabao mawili kwenye mchezo huo.

Liverpool waliipiku Arsenal kwenye nafasi ya pili, baada ya kikosi hicho cha Arsene Wenger, kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Everton juzi Jumanne usiku.

Baada ya kikosi cha Man City kinachonolewa na kocha Pep Guardiola kufungwa mechi mbili mfululizo dhidi ya Chelsea na Leicester City, juzi Jumatano kiliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Watford, wafungaji wakiwa ni Pablo Zabaleta na David Silva.

Lakini ushindi huo uliingia dosari baada ya kiungo Ilkay Gundogan kupata majeruhi ya goti ambayo Guardiola amesema yatamweka nje kwa muda, huku City wameachwa pointi saba na vinara wa ligi, Chelsea, wakiwa nyuma ya Liverpool na Arsenal kwa pointi moja.

Tottenham waliendelea kujikita nafasi ya tano baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Hull City, wakati Christian Eriksen, alipasia nyavu mara mbili na Victor Wanyama mara moja.

Baada ya kuichapa Spurs bao 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, United waliweka rekodi ya kushinda mechi ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Agosti mwaka huu, lakini waliendelea kubaki nafasi yao ya sita wakipitwa pointi tatu na kikosi cha Mauricio Pochettino, Spurs.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -