Tuesday, October 27, 2020

CHELSEA BILA KANTE, COSTA INAWEZEKANA?

Must Read

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo,...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City...

*Wote wana kadi za njano tano

*Kuikosa mechi ya Bournemouth

LONDON, England

Chelsea watawakosa wachezaji wao wawili muhimu kwenye mchezo ‘Boxing Day’, baada ya Diego Costa na N’Golo Kante kuonyeshwa kadi ya njano ya tano kila mmoja kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Crystal Palace.

Wawili hao wataikosa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Bournemouth siku ya pili ya Sikukuu ya Krismasi (Boxing Day), baada ya kadi hizo za njano walizoonyeshwa katika mchezo wa Ligi Kuu England walioshinda bao 1-0 na kumwacha kocha wao Antonio Conte njiapanda.

Kutokana na umuhimu wao kwenye kikosi hicho, je, Chelsea itawezekana kuendeleza rekodi za ushindi bila ya nyota hao wawili? Conte atapangaje timu yake bila ya wachezaji hao?

Katika mchezo huo dhidi ya Crystal Palace, Costa alifunga bao lake la 13 msimu huu wa Ligi Kuu England katika Uwanja wa Selhurst Park na kuisaidia klabu yake ya Chelsea kushinda mechi ya 11 mfululizo. Pia bao hilo lilimfanya mshambuliaji huyo aipiku rekodi yake ya mabao ya msimu uliopita.

Conte amemzungumzia Costa kama ‘askari’ na kinara huyo wa mabao ameanza mechi zote za Ligi Kuu England msimu huu. Hakuna kama yeye atakayeweza kuziba pengo lake. Ingawa adhabu hiyo ya Costa itampa nafasi Michy Batshuayi. Nyota huyo, Batshuayi aliyenunuliwa kwa pauni milioni 33.2 majira haya ya kiangazi, amekuwa akicheza mechi za EFL Cup na kuingia mechi kadhaa za ligi akitokea benchi, hivyo atataka kuonyesha nini anaweza kufanya.

Nyota huyo wa Ubelgiji, Batshuayi aliyefunga mabao 23 katika mechi 50 alizochezea Marseille kwenye michuano mbalimbali msimu uliopita, lakini ana bao moja Ligi Kuu England akiisadia Chelsea kushinda dhidi ya Watford, Agosti mwaka huu.

Chipukizi wa England mwenye umri wa miaka 19, Dominic Solanke, ndio mshambuliaji wa Chelsea ambaye hajacheza, lakini Pedro, Eden Hazard na Cesc Fabregas wanaweza wakacheza kama namba tisa ‘feki’ ili Conte aweze kuendelea na mbinu zake.

Kwa upande wa pengo la Kante ambaye aliisadia Leicester City kunyakua taji msimu uliopita akiwa ameshinda mechi nyingi tangu msimu uliopita na huu pia, amekuwa msaada mkubwa kwa Chelea katika mbio za ubingwa baada ya kumbeba Claudio Ranieri.

Nyota huyo wa Ufaransa, Kante ni mmoja wa wachezaji watano walioongoza kwa kupora mipira na kuvuruga pasi msimu uliopita, msimu huu amesaidia kulinda safu ya ulinzi ya Chelsea na kumfanya Conte kuwa na safu nzuri ya ulinzi.

Unawezaje kuziba pengo la ‘mkata umeme’ wa Chelsea? Huenda Conte akamtumia Cesc Fabregas. Nyota huyo wa Hispania ana uwezo mkubwa wa kutengeneza pasi za mwisho kuliko kulinda, lakini akicheza pamoja na ‘pacha’ wa Kante, Nemanja Matic, ambaye amerejea kwenye kiwango chake kilichoipa Chelsea ubingwa msimu wa 2014-15, Conte anaweza kumtegemea nyota huyo wa Serbia, Matic kuvuruga mashambulizi ya Bournemouth.

Nyota ambaye kwa sasa hana nafasi Chelsea, John Obi Mikel huenda akawa ndio mchezaji pekee wa kuziba pengo la Kante, wakati chipukizi Nathaniel Chalobah na Ruben Loftus-Cheek wanaweza wakapata nafasi. Lakini Fabregas ambaye alicheza vizuri na Matic msimu wa 2014-15, anaonekana kama ndio chaguo na ataongeza nguvu kwenye mashambulizi kwenye kikosi cha Chelsea ambao wameshinda mechi zao tatu mfululizo kwa bao 1-0.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Manispaa...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -