Wednesday, January 20, 2021

CHINESE SUPER LEAGUE LIGI YA VIGOGO WATAMU WA PESA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

HAISHANGAZI siku hizi kusikia mchezaji nyota akiondoka katika klabu kubwa nchini England au hata Hispania na kusajili na klabu fulani nchini China. Japo inaonekana kama wachezaji wanaomaliza muda wao wa soka ndio huenda kumalizia soka lao nchini humo, lakini ukweli kwa sasa unabadilika taratibu kwani pamoja na kusajili wachezaji wanaoonekana kuanza kuchoka, lakini fedha wanazolipwa wachezaji katika ligi ya China si za kitoto.

Ligi hii licha ya kuwapo kwa muda lakini unaweza kusema ni ligi chini ya Chama cha Soka cha China (Chinese Football Association), Ligi Kuu ya China maarufu kama Chinese Super League (CSL) inaonekana kama ni ligi changa masikioni mwa wapenzi wa soka hasa kutokana na kutokuwa maarufu sana. Kwa sasa inapata umaarufu mkubwa hasa baada ya timu za China kuanza kusajili wachezaji wakubwa wenye majina ya kiwango cha dunia.

Kwa sasa inajulikana kama Ping An Chinese Football Association Super League, ikiwa imenogeshwa vyema na udhamini mnono wa mabilioni ya fedha, udhamini ambao ni mkubwa kuliko wa ligi yoyote ya soka barani Asia.

Ligi hii ilianza rasmi mwaka 2004 baada ya kubadilishwa kutoka Ligi Daraja la Kwanza iliyojulikana kama Chinese Jia-A League na ilianza kwa kuwa na timu 12 kabla ya kuongeza timu nyingine na kuwa 16. Lakini miamba inayotingisha kwenye ligi hiyo hadi hivi sasa ni pamoja na matajiri wa kutupwa na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Guangzhou Evergrande, ambao wao tangu walipopanda daraja msimu wa 2011 wamekuwa mabingwa hadi sasa.

Cligi ya China inaendeshwa chini ya kampuni maalumu ya CSP Company  ambayo inaendesha ligi kibishara na klabu zote shiriki zinakuwa wabia kwa maana kwamba kila msimu klabu zote zinakuwa wanahisa na kila mwisho wa msimu klabu zinapata gawio lao kulingana na hisa walizonunua. Ni utaratibu mpya ambao unaifanya ligi hii kuendeshwa kisasa zaidi ya ligi zote za soka duniani.

CSL ni tofauti na ligi nyingine, kwanza yenyewe huanza Februari au Machi na humalizika Novemba au Desemba kila msimu. Na timu zote kucheza kwa mzunguko wa nyumbani na ugenini. Kwa sasa ni ligi yenye mechi 240 ikiwa ni mechi chache kulinganisha na ligi nyingine maarufu barani Ulaya. Timu mbili za mwisho hushuka daraja hadi China League One, ambapo mbili kutoka ligi hiyo ya chini kupanda CSL.

Timu tatu za juu za CSL na bingwa wa Chinese FA Cup (CFC) huenda kushiriki michauno ya kimataifa hasa AFC Champions League ligi ya mabingwa Bara la Asia na mshindi wa nne wa ligi na mshindi wa pili wa CFC, huenda kwenye michuano ya kimataifa ya Asia kwa kuanzia ngazi ya mchujo.

Ilikotoka CSL

Mwaka 1994, China ilifanya mapinduzi ya mfumo katika sekta ya michezo ambapo kwenye soka walianza mfumo wa soka la kulipwa na iliyokuwa ligi ya China wakati huo Chinese Jia-A League,  ilikuwa ligi ya kwanza ya kulipwa nchini humo. Ligi hiyo ilipata mafanikio makubwa ya ndani lakini kulikuwa na changamoto kubwa ya kiuendeshaji ambayo masuala ya kubeti yaliiharibu kabisa ligi hiyo na ikatawaliwa kwa kiasi kikubwa na upangaji wa matokeo na ununuaji wa mechi pamoja na rushwa.

Serikali iliingilia kati na hatimaye Chama cha Soka cha China kikaamua kubadili mfumo mzima wa uendeshaji wa ligi hiyo ikiwa sambamba na kupiga marufuku kampuni za kubeti. Hapo ndipo ilizaliwa CSL, mwaka 2000 CFA walitangaza mabadiliko ya mfumo wa ligi hiyo na miaka minne baadaye mfumo ulipitishwa ukiwa na sheria nzito ambazo hazitoi nafasi kwa timu kupanga matokeo wakarushwa kwenye mechi za CSL.

Miamba 16 ya CSL msimu wa 2017

  1. Beijing Guoan F.C, timu hii maskani yake ni kwenye dimba la Workers Stadium lenye uwezo wa kubeba mashabiki 66,000, inapatikana kwenye Wilaya ya Chaoyang jijini Beijing, haijawahi kushuka daraja tangu msimu wa 2004 na ilishatwaa ubingwa wa CSL mara moja kwa 2009.
  2. Changchun Yatai. Hii ni timu inayopatikana katika mji mdogo wa Changchun, uwanja wake ni Development Area Stadium wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 25, ilitwaa taji la CSL mara moja mwaka 2007 msimu mmoja baada ya kupanda daraja.
  3. Chongqing Lifan, inapatika mjini Chongqing na uwanja wake ni Chongqing Olympic Sports Center wenye uwezo wa kubeba mashabiki 58,000, ni timu ambayo imekuwa ikipanda na kushuka kwenye ligi hiyo.
  4. Guangzhou Evergrande Taobao; hawa ndio vigogo hasa wa ligi ya China, wanapatikana katika mji wa Guangzhou na maskani yao ni Uwanja wa Tianhe Stadium wenye uwezo wa kubeba mashabiki 58,500, walipanda ligi kuu msimu wa 2008 lakini wakashuka msimu wa 2009, wakapanda tena msimu wa 2011 na tangu hapo wao ni mabingwa kwa zaidi ya miaka sita (6) na hawajawahi kushushwa.
  5. Guangzhou R&F, inapatikana katika mji wa Guangzhou, Guangdong na uwanja wake wa nyumbani ni Yuexiushan Stadium unaoingiza mashabiki 30,000 imekuwa ikipanda na kushuka kwenye CSL.
  6. Guizhou Hengfeng Zhicheng. Inapatikana katika mji mdogo wa Guiyang, uwanja wake wa nyumbani ni Guiyang Olympic Sports Center unaoingiza mashabiki 52,000 tangu ilipopanda mwaka 2007 haijashuka daraja.
  7. Hebei CFFC. Inapatikana katika mji wa Qinhuangdao, Hebei, uwanja wake wa nyumbani ni Qinhuangdao Olympic Sports Center Stadium, unaiongiza mashabiki 3,357 imepanda kwenye ligi ya CSL mwaka huu na sasa inajipanga kwa ajili ya msimu wake wa pili kwenye ligi hiyo.
  8. Henan Jianye, maskani yake ni katika mji wa Zhengzhou kwenye Jimbo la Henan, uwanja wake ni Zhengzhou Hanghai Stadium wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 29,800 ilipanda CSL mwaka 2007 kabla ya kushuka na kupanda tena 2012 hadi hivi sasa.
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -