Saturday, October 31, 2020

CHIPUKIZI BONGO WAMPASUA KICHWA KASSIM MGANGA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SHARIFA MMASI


MOJA ya vitu vikubwa vinavyowatia joto nyota wakongwe katika muziki wa Bongo Fleva nchini, ni kuibuka kwa kasi kwa wasanii chipukizi ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri.

Mmoja wa nyota ambao wameeleza hofu yao ya wazi kwa wasanii chipukizi ni Kassim Mganga, ambaye anasema kuendelea kuibuka kwa wasanii chipukizi kunampasua kichwa isivyo kawaida.

Anasema pamoja na kumpasua kichwa kwa ufanisi wa kazi, lakini pia wanamuumiza kichwa kutokana na kwamba wengi wanahitaji sana msaada wa wasanii hao wakongwe.

“Hili lipo wazi kabisa kwa kila mmoja wetu, kwani vilio vya wasanii wachanga kuhitaji msaada wa wakongwe ili nao wakanyage pale walipopita vimekuwa ni wimbo wa kila siku,” anasema.

Je, kwanini Kassim Mganga ameamua kufunguka?

Jina la Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ si geni masikioni mwa wapenzi wa muziki nchini, kutokana na umaarufu aliowahi kupata miaka ya nyuma kupitia kazi zake za muziki.

Dudu Baya ambaye aliwahi kutamba na ngoma kibao ikiwamo ‘Kikongwe’, ‘Dege la Jeshi’ na nyingine nyingi kwa sasa amepotea kwenye soko la muziki kutokana na kuibuka kwa vipaji vipya vinavyokwenda na wakati.

Achilia mbali Dudu Baya, yupo yule aliyewahi kuwa kidume wa muziki Tanzania, 20 Percent ambaye kazi zake za muziki mzuri zilimfanya anyakue tuzo  tano za Kili Music naye kwa sasa amepotea.

Tuzo alizopata msanii huyo ziliamsha hisia za mashabiki wake ambao waliendelea kutoa ushirikiano kwa kazi zake. Ukweli ni kwamba, 20 Percent alitesa katika kipindi hicho ambacho ushindani wa soko la muziki ulikuwa mkubwa.

Pamoja na umaarufu aliowahi kuupata miaka hiyo kupitia ngoma zake kibao ikiwamo ‘Money Money’, kwa sasa jina la mkali huyo halitajwi mara kwa mara kwenye anga la muziki wa kibongo.

Orodha ya wasanii waliowahi kupagawisha mashabiki ipo kubwa sana, waliotajwa hapo juu ni ni mfano tu  wa wengi  na jambo hili ndiyo ambalo pengine linamnyima raha Kassim Mganga.

Hiyo ilikuwa ni juzi na jana ya ukumbusho wa baadhi ya wasanii waliowahi kutikisa soko la muziki Tanzania, lakini tukirudi upande wa leo yetu tulionayo, wasanii mbalimbali wamefanikiwa kuliteka soko la muziki ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa wakali hao yupo Nasseb Abdul ‘Diamond’, Ally Kiba, Kassim Mganga, Lady Jaydee, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, Linah Sanga, Baraka Da Prince na wengine wengi.

Kupitia wasanii hao, Kassim Mganga anawakumbusha wadau wa muziki kwamba wakongwe wote wa kazi hizo ambao kwa sasa hawasikiki, waliwahi kulikanyaga zulia ambalo wamelikalia wao hivi sasa.

“Hapa tulipo sisi wasanii wa Bongo Fleva tunaotamba sokoni, wale wa Singeli, Taarabu, hip hop na muziki mwingine, tukumbuke kuwa wapo wakali waliowahi kutamba zaidi yetu.

“Itafikia siku na sisi  tukazidiwa nguvu na chipukizi,” anasema Kassim Mganga ambaye aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwamo ‘Awena’.

Kassim anasema ni vema wasanii maarufu wazinduke na kuchukua hatua ya kuwasaidia chipukizi kwa kuwaonyesha njia sahihi za kupita ili nao waje kuleta heshima kwenye soko la muziki hapo baadaye.

“Ni ukweli usiofichika wasanii wachanga wanataabika sana hapa nyumbani, wakongwe kwenye hili gamu tunajifanya kama hatuwaoni vile na inapotokea wanahitaji msaada kwetu bado tunawatolea nje jambo ambalo linaweza kutuweka pabaya siku sijazo,” anasema.

Kassim anasema anaamini chipukizi wengi wana uwezo mkubwa sana endapo watapata usimamizi mzuri kutoka kwa wakongwe wa kazi za muziki.

Anasema kwa upande wake, mpaka sasa ana zaidi ya wasanii 100 aliyowahi na anaendelea kuwasaidia na anatoa wito kwa wasanii wakubwa kujitokeza kusaidia kuinua vipaji vya chipukizi ili waje kuleta mapinduzi makubwa kwenye soko la muziki wa Afrika hapo baadaye.

“Natoa wito kwa wasanii wakubwa wanaotamba hapa nchini kwa sasa, tujitokeze kuwanyanyua chipukizi ili miaka ya baadaye waje kututoa kimasomaso kwenye tuzo za Afrika na dunia kwa ujumla,” alisema Kassim.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -