Thursday, December 3, 2020

CHIRWA AMRUDISHA PLUIJM YANGA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

MABAO ya ufundi wa hali ya juu yaliyofungwa na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Kiluvya United yanaonekana kumrejesha karibu na aliyekuwa kocha na mkurugenzi wa zamani wa timu hiyo, Hans van der Pluijm.

Pluijm aliyeiwezesha Yanga kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara misimu miwili, ameondoka baada ya uongozi wa klabu hiyo kusitisha mkataba wake wiki iliyopita.

Chirwa ameweka rekodi ya kwanza msimu huu katika michuano ya Kombe la FA, baada ya juzi kupiga hat-trick dhidi ya Kiluvya wakati Yanga wakishinda mabao 6-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kutinga robo fainali na sasa itakutana na Prisons katika hatua hiyo.

Straika huyo Mzambia aliifungia timu yake katika dakika ya 24, 45, 70 na 86 na kumfanya Pluijm aliyekuwa jukwaani kushuhudia mchezo huo kushangilia na kuonekana mwenye furaha muda wote wa mchezo huo.

Pluijm ambaye alikuwa amekaa pembeni mwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, muda wote walionekana kufurahishwa na namna Yanga ilivyokuwa ikicheza na jinsi Chirwa alivyokuwa akipachika mabao hayo kwa ustadi mkubwa.

Moja kati ya mabao ambayo yalimkuna Pluijm ni bao la nne alilolifunga kwa ustadi mkubwa, baada ya kupokea krosi kutoka upande wa kulia mwa uwanja iliyopigwa na winga Simon Msuva kisha kuunganisha juu kwa juu nyavuni.

Baada ya kuingia bao hilo, Pluijm alionekana kuwa na tabasamu kubwa huku akimweleza jambo Mkwasa.

Baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo, Pluijm aliliambia BINGWA anafurahishwa na Yanga na katika mchezo huo ameguswa zaidi na uwezo wa Chirwa ambao umeimarika sana lakini hawezi kuzungumzia zaidi masuala ya mchezo huo au yanayoihusu Yanga.

“No, nimekuja kuangalia mpira, kuiangalia timu ninayoipenda, siwezi kuzungumzia masuala ya kiufundi ya Yanga, lakini kama shabiki na mpenzi wa mpira nimefurahishwa na namna ya Chirwa alivyofunga,” alisema Pluijm.

Chirwa alisajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita akitoka FC Platinum ya Zimbabwe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -