Sunday, November 1, 2020

CHIRWA AMSOGEZA AJIBU KWA MASHABIKI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MAREGES NYAMAKA NA WINFRIDA MTOI

KUIBUKA kwa mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ambaye amecheka na nyavu katika mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kuanza nyodo, kumewaibua wenzao wa Simba ambao wameonekana kumkabidhi mikoba mkali wao, Ibrahim Ajib,  wakiamini ndiye mwenye uwezo wa kuwasambaratisha watani wao hao wa jadi.

Ajib ni moja wa mastraika vipenzi wa Simba wakiamini ana uwezo wa kufanya lolote uwanjani iwapo ataamua, lakini pia atajengewa mazingira stahiki ya kufanya mambo yake.

Ni kutokana na hilo pamoja na wapenzi wa Yanga kutamba kuwa Chirwa ameanza vitu vyake, wenzao wa Msimbazi wameonekana kuwacheka wakiamini kuwa Mzambia huyo si lolote mbele ya Ajib, mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, lakini pia mbinu za kimchezo.

Ajib alithibitisha hilo Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, pale alipoifunga Majimaji ya huko na hivyo kujibu mapigo kwa Chirwa aliyezitikisa nyavu za Stand United Ijumaa, siku moja kabla ya Simba kuwanyuka wenyeji wao 3-0.

Mwisho wa siku, wakati mashabiki wa Yanga wakitamba kuwa Chirwa ameanza kufanya vitu vyake, wenzao wa Simba wanawajibu wakitamba kuwa Ajib karudi.

Juma Masood ni shabiki wa Simba ambapo katika mahojiano na BINGWA jana, alisema: “Hawa Yanga walikuwa wanatusumbua sana mtaani kuhusu huyo Chirwa wao, kisa kafunga michezo miwili mfululizo, nadhani wameuona moto wa Ajib kule Songea.”

Kwa upande wake, shabiki wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Khatibu wa Mbezi, Dar es Salaam, alitanba: “Chirwa huwezi kumfananisha na Ajib kwani ana uwezo mkubwa wa kufunga na ana mabao mengi zaidi.”

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Februari 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo ndipo itakapofahamika kuwa nani ni zaidi baina ya Chirwa na Ajib.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -