Friday, December 4, 2020

CHONDE CHONDE WAAMUZI PAMBANO LA WATANI LEO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

WATANI wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga, wanatarajia kukutana leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kipute hicho cha kukata na shoka kinatarajiwa kuwa cha aina yake kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo mbili, lakini zaidi ikiwa ni mbio za ubingwa kwa wakati huu ambao timu hizo zinafukuzana kileleni.

Wakati Simba wakiongoza ligi kwa pointi zao 51 kutokana na mechi 22 walizocheza, Yanga wapo nafasi ya pili na pointi zao 49, lakini mabingwa watetezi hao wakiwa na mechi moja mkononi dhidi ya watani wao.

Ni kutokana na hali hiyo, pambano hilo la watani linaonekana kuvuta hisia za wengi kuanzia ndani hadi nje ya Tanzania, kutokana na historia yao ya upinzani wa jadi lakini pia zikiwa ndizo zenye mashabiki wengi zaidi.

Kikubwa katika mchezo huo, mashabiki watakuwa na hamu kuona ni timu gani inamtambia mwenzake, lakini pia wachezaji gani watakaong’ara, iwe ni wale wazawa au wale wa kigeni.

Yote kwa yote, wengi watamiminika kwa wingi uwanjani au kuufuatilia kwa karibu mchezo huo kupitia runinga, wakitarajia kupata bonge la burudani kutoka kwa wachezaji wao kila upande ukijivunia kufanya usajili wa nguvu.

Pamoja na matarajio hayo ya mashabiki, mwisho wa siku BINGWA tunaamini waamuzi ndio watakaoamua watu watoke vipi uwanjani, yaani wawe wameridhika na ushindi au kipigo walichopata au la.

Tunasema hivyo kutokana na uzoefu tulionao kwani mara nyingi timu za Simba na Yanga zinapopambana, waamuzi huwa wanaboronga mno na kuwanyima mashabiki burudani waliyoitarajia.

Wakati mwingine wapo wanaoboronga kutokana na kuchanganyikiwa na ukubwa wa mchezo huo, presha kutoka kwa wachezaji, huku wakati mwingine ikidaiwa waamuzi husika kurubuniwa na viongozi wa upande mmoja.

Hivyo basi, tunapolisubiri kwa hamu pambano hilo la watani wa jadi, tuwaombe waamuzi kuchezesha kwa kufuata sheria zote 17 za soka bila kupendelea upande wowote.

Kama kila mmoja wetu anavyofahamu, waamuzi ni sehemu muhimu mno ya mchezo wowote wa soka, inapotokea wanaboronga, madhara yake ni makubwa mno kuanzia kwenye matokeo ya mechi husika, usalama wao na mashabiki, lakini pia kwa majaliwa ya soka na wachezaji wetu kwa ujumla.

Hivyo ni matumaini yetu waamuzi

watakaochezesha pambano la watani leo,

watatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kufuata sheria zote 17 za mchezo huo na mwisho wa siku kupata mshindi atakayestahili kulingana na kile wachezaji wake walichokifanya uwanjani na si vinginevyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -