Saturday, October 31, 2020

COASTAL YAKUBALI YAISHE DARAJA LA KWANZA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

COASTAL Union wamekubali yaishe baada ya kukata tamaa kwa timu yao kuweza kurejea Ligi Kuu msimu ujao kutokana na kufanya vibaya mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Klabu ya Coastal Union, Hafidhi Kidoh, alisema hawana nafasi ya kurejea kwenye ligi hiyo kutokana na nafasi wanayoshika kwenye kundi lao.

Kidoh alisema mipango ya kuirejesha  Coastal Union Ligi Kuu ipo, lakini kwa msimu huu wameshindwa kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri.

“Mipango yetu mikubwa ilikuwa ni kuhakikisha tunairejesha timu hii Ligi Kuu msimu huu, lakini kutokana na kuwepo kwa matokeo yasiyoridhisha kwa baadhi ya michezo yetu itatulazimu kusubiri mpaka msimu ujao,” alisema Kidoh.

Alisema kwa sasa wanachokifanya ni kuhakikisha wanaweka mipango imara ya kuweza kushinda michezo yao inayofuata ili wasiendelee kushuka daraja.

Kidoh alisema wachezaji wao wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Kurugenzi ya Mufindi utakaochezwa Januari 8 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa.

Alisema wachezaji hao wanaendelea na mazoezi asubuhi na jioni chini ya kocha wao, Mohamed Kampira, katika viwanja vya Amboni jijini Tanga ili waweze kumaliza katika nafasi nzuri.

Kidoh alisema malengo yake ni kutaka kushinda dhidi ya Kurugenzi, licha ya kwamba hawana matumaini ya kurejea Ligi Kuu Bara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -