Sunday, January 17, 2021

CONTE ASIDANGANYWE NA TABASAMU LA ABRAMOVICH

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Antonio-Conte

NA AYOUB HINJO

MTAZAME Antonio Conte vizuri. Usimtazame kwa jicho la kawaida kabisa, mwangalie kisha iulize nafsi yako kama atakuwa kwenye mikono salama msimu ujao. Hali yake si nzuri, moyo wake unasononeka.

Kuna mambo mengi yanazunguka nyuma yake ambayo si rahisi kuyaona kwa macho. Kuna mambo yanafanyika ambayo yanaonekana kukwamisha kazi yake kiutendaji.

Msimu wa 2014/15 timu ya Chelsea walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England. Ilikuwa timu ya kuogopwa kweli, walikuwa kundi moja na hatari kwa wapinzani.

Aina ya mpira waliocheza, mbinu zilizotumika na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ilikuwa funguo ya mafanikio kwenye msimu ule ambao Jose Mourinho alionekana kubadilika kidogo.

Msimu uliofuata kila mtu anajua kilichowakuta. Hawakuwa kitu kimoja tena, kila mmoja alifanya kila kitu anavyojua. Timu yote ilivurugika, mwishowe walimaliza msimu katika nafasi ya 10. Huku Mourinho akifukuzwa kwa mara nyingine tena.

Ilionekana itakuwa ngumu kwa Conte kuiunganisha timu hiyo iliyoonekana kupotea msimu mmoja nyuma. Jambo bora alifanikiwa kurejesha imani ya kila mchezaji pia aliweza kuwaunganisha na kuwa kitu kimoja.

Conte alionekana mshindi kwa kila alichokifanya, kila kitu kiligeuka dhahabu kwake. Hakika hata mashabiki wa Chelsea walitembea vifua mbele, huku wakiimba jina lake.

Msimu mpya unaanza leo, lakini Conte haonekani kuwa na furaha kabisa. Nafsi yake imepunjwa amani na upendo ambao aliupata msimu uliopita, anaonekana amekata tama japo ni mapema kumzungumzia vibaya.

Chelsea ni timu ambayo haiwezi kuvumilia makocha pindi inapofanya vibaya. Ni ngumu kuwa kwenye timu hiyo hata kama ulifanya vizuri miezi 12 iliyopita. Kinachoangaliwa sasa unafanya nini na timu inapata nini chenye manufaa.

Dirisha la usajili litafungwa Agosti 31, lakini Conte haonekani kufurahia usajili ambao unafanywa na timu yake. Wamefanya usajili mzuri lakini amekosa wachezaji ambao alikuwa anawahitaji.

Romelu Lukaku alikuwa chagua lake la kwanza katika idara ya ushambuliaji ili achukue nafasi ya Diego Costa ambaye ameonyeshwa mlango wa kutokea kwenye timu hiyo.

Lukaku ni mchezaji wa Manchester United sasa, ni moja ya vitu ambavyo Conte vimemuacha mdomo wazi kwa mshangao ni jinsi gani wamemkosa kizembe mchezaji huyo.

Conte kamsajili Alvaro Morata kutoka Real Madrid. Tayari mashabiki wa timu hiyo wameanza kuwa na mashaka na mchezaji huyo. Licha ya ugeni wake ameshindwa kuonyesha kiwango kizuri katika michezo ya ‘pre season’.

Alex Sandro beki wa kushoto wa Juventus pia ameshindwa kujiunga na timu hiyo. Hilo pia limemuacha njia panda, asijue cha kufanya huku akiugulia moyoni.

Wamemuuza Nemanja Matic moja mchezaji aliyetoa msaada mkubwa msimu uliopita hususani katika mbio za ubingwa ambazo walifanikiwa kuzimaliza wakiwa mabingwa .

Wamepoteza mchezaji bora kwenye kikosi chao lakini nafasi yake imechukuliwa na Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco. Swali ambalo lipo, kama Bakayoko ataweza kuziba nafasi hiyo kikamilifu zaidi na mwisho wa siku mashabiki wamsahau kabisa Matic.

Msimu mpya ambao unakaribia kuanza utawafanya Chelsea washiriki michuano mingi tofauti na msimu uliopita ambao walikuwa wanashiriki michuano ya ndani tu.

Wasiwasi upo kwa tajiri wa timu hiyo na bodi yake, kuhusu kocha huyo. Wamekuwa hawana uvumilivu pindi makocha wanavyofanya vibaya. Mara zote huwa wanafukuzwa.

Carlo Ancelotti alifukuzwa msimu mmoja baada ya kuipa makombe Chelsea. Mourinho alifukuzwa baada ya kuipa ubingwa Chelsea mara zote mbili. Sasa Conte ni nani asifukuzwe kama timu ikifanya vibaya? Hilo ni jambo gumu kwa Abramovich.

Hatma ya Conte ipo miguuni mwa wachezaji wake. Dhamana ya kusalia kwenye timu hiyo wameibeba wachezaji wa timu hiyo. Kama wakiamua kumzamisha, hatokuwa salama lakini ikiwa kinyume na hapo maisha yataonekana mazuri kwake.

Ni vipi msimu mpya Conte atawapanga wachezaji wake? Hilo ndio jambo bora ambalo anapaswa kulijua hasa katika msimu wake wa pili. Hakuna jinsi maisha yake yanaonekana yapo shakani sasa.

Mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Arsenal ulikuwa kioo kwake cha kujitazama tena jinsi atakavyoianza ligi tena. Hakika unaweza kuwa msimu mgumu kwa Conte, naamini kila timu itakuwa imetafuta mbinu za kupambana na Chelsea kwa mfumo ule wa 3-4-3.

Nini Conte amepanga kufanya msimu ujao kwa Chelsea. Nini amepanga kwa ajili ya kutetea ubingwa wake na kushiriki michuano ya Ulaya, UEFA.

Ni wazi Conte hakuwahi kufanya vizuri kwenye michuano ya Ulaya, UEFA kwa msimu ujao anaonekana ataelekeza nguvu huko ili kuiwezesha timu hiyo kushinda kombe hilo.

Yote kwa yote Conte inabidi atambue kisu cha Conte kinamsubiri pindi atakavyofanya vibaya. Bosi hana muda wa kupoteza pindi anapotazama uwekezaji wake hauendi sawa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -