Friday, December 4, 2020

Costa amekuja kwa kazi moja tu England

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

ALIPOKAMILISHA dili la kutua Chelsea akitokea Atletico Madrid, mshambuliaji wa Hispania mwenye uraia wa Brazil, Diego Costa, alionekana mwenye furaha ya kuichezea timu hiyo yenye makazi yake jijini London.

Costa alihamisha mapenzi yake kwa Chelsea na akajitoa kwa moyo wote kuhakikisha inafanya vizuri.

Kazi yake kubwa ni kucheka na nyavu na ameifanya kwa moyo wote, bila kuwapunja furaha mashabiki wa Chelsea. Hiyo haitoshi, ameifikia rekodi ya kufunga mabao 40 kwa haraka pale England.

Costa alifanikiwa kuingia kwenye orodha ya washambuliaji waliofunga mabao 40 kwa haraka zaidi wakati timu yake ilipokuwa ikikabiliana na Southampton wikiendi iliyopita kwa kufunga bao la ushindi kwa timu yake.

Bao hilo pia liliisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa nne mfululizo katika ligi bila kufungwa bao lolote.

Mchezo huo ulikuwa ni wa 64 wa Ligi Kuu England kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28.

Costa alifanikiwa kuifikia idadi hiyo ya mabao kutokana na jitihada zake zilizomfanya aizoee ligi ya nchini humo licha ya matukio kadhaa ya utovu wa nidhamu aliyoyafanya.

Ni washambuliaji watano pekee waliofunga mabao 40 katika michezo michache zaidi ya Costa, ambapo Andy Cole na Alan Shearer walifikia idadi hiyo ya mabao ndani ya michezo 45 tu ya ligi.

Cole alifikisha mabao 40 akiwa na jezi ya Manchester United iliyomsajili mwaka 1995 akitokea Newcastle United (huko ndiko mabao 40 yalipoanza kuhesabiwa).

Shearer alifunga jumla ya mabao 112 akiwa Blackburn kabla ya kutua Newcastle kwa ada ya pauni milioni 15 mwaka 1996.

Mpachika mabao wa zamani wa Sunderland, Kevin Phillips alifunga mabao hayo 40 ndani ya mechi 67. Phillips aling’ara zaidi pale Sunderland ilipopanda Ligi Kuu England mwaka 1999.

Kwenye msimu wake wa kwanza ligi kuu, Phillips alifunga jumla ya mabao 30 ambapo alimaliza msimu na tuzo ya kiatu cha dhahabu England na kile cha Ulaya huku msimu wake wa pili akifunga mabao 11.

Wachezaji wengine wawili ambao walifunga mabao 40 ndani ya michezo michache, ni Mholanzi Ruud van Nistelrooy wa Man United na straika wa Kihispania, Fernando Torres aliyekuwa akiichezea Liverpool.

Torres na Nistelrooy walipachika mabao hayo ndani ya mechi 60.

Aidha, Costa amewapiku wachezaji nyota wa klabu kubwa za Ligi Kuu England kama vile Sergio Aguero wa Man City ambaye amefunga mabao 40 ndani ya mechi 71 huku Thierry Henry aliyewahi kukipiga Arsenal akishikilia rekodi ya kufunga mabao hayo kwenye michezo 73.

Wanaokamilisha orodha hii ya wafungaji bora wa mabao 40 ni mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane na Teddy Sheringham aliyewahi kuitumikia Man United. Hawa wote wamefunga mabao 40 ndani ya michezio 74 ya Ligi Kuu England.

Costa atakuwa na nafasi nyingine ya kuongeza mabao hayo atakapokutana na Everton wikiendi hii na ikumbukwe kwamba mshambuliaji huyo tayari ameifunga timu hiyo mabao matatu katika michezo minne waliyokutana kabla ya mtanange wao huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -