PARIS, Ufaransa
STAA wa Manchester United, Paul Pogba, amefurahishwa kuona ushangiliaji wake, maarufu ‘dab’, ukitumika kama swali la hisabati na mwalimu mmoja huko Ufaransa.
Baada ya kuona picha yake akishangilia kwa ku-dab ikitumika kama kanuni ya ‘Pythagoras’, Pogba aliandika kwenye twitter akijivunia suala hilo.
Swali hilo liliunganishwa na picha ikimuonesha Pogba akishangilia huku mikono yake ikichorwa kwa mfano wa pembetatu mbili.