Sunday, November 29, 2020

DAKIKA 7 ZA NYONGEZA, SIMBA SC YAREJEA KILELE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

KAULI ya kujitamba ya Msemaji wa Simba, Haji Manara, akisema: “This is Simba” (Hii ni Simba), imeonekana jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, baada kikosi hicho kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuibuka na  ushindi wa 3-2 dhidi ya Mbao FC na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo, Simba ilitumia vizuri dakika saba za nyongeza kwa kusawazisha na kupata bao la ushindi kwa mabao mawili yaliyofungwa na Fredrick Blagnon, huku Mzamiru Yassin akitupia la ushindi.

Mbao walianza kwa kutawala tangu dakika za mwanzo wa mchezo huo, huku Simba wakionekana kulemewa eneo la kiungo kutokana na kumkosa nahodha wao, Jonas Mkude ambaye alikuwa akitumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano.

Mbao walitumia vizuri udhaifu wa Simba ulioonyeshwa mwanzoni mwa mchezo na kupata bao dakika ya 18 lililofungwa na George Sangija kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango, Peter Manyika.

Wakati Simba wakijipanga ili kusawazisha bao hilo, Sangija aliongeza bao la pili dakika ya 33, baada ya mabeki wa Simba kushindwa kujipanga vizuri.

Simba walijaribu kugangamala na kufanya mashambulizi likiwamo lile la dakika ya 23, ambapo shuti la beki wa kushoto wa timu hiyo, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kutoka nje, kabla ya mshambuliaji Juma Luizio kupiga shuti lililopita pembeni kidogo ya goli dakika chache kabla ya mapumziko.

Kocha wa Simba, Joseph  Omog ambaye aliwaacha benchi wachezaji wake muhimu kama mlinda mlango, Daniel Agyei, washambuliaji Leudit Mavugo, Ibrahim Ajib na kiungo Said Ndemla, aliamua kufanya mabadiliko kabla ya mapumziko na kuwaingiza Ndemla na Mavugo kabla ya mapumziko na kuwatoa beki, Hamad Juma na Pastory Athanas.

Kipindi cha pili alimpumzisha Juma Luizio na kumwingiza Blagnon ambao wote walifanya Simba kupata nguvu na kuishambulia Mbao wakati wote na kupoteza nafasi kadhaa.

Dakika ya 82, bidii na juhudi zao zilizaa matunda na kupata bao la kwanza lilofungwa na Blagnon kwa kichwa akiunganisha mpira mrefu wa James Kotei na kuonekana kama mchezo ungemalizika kwa Mbao kushinda 2-1.

Lakini badala yake Simba ilizidi kucharuka hasa baada ya kibao cha mwamuzi wa akiba kuonyesha dakika saba za nyongeza, ambapo Blagnon alifunga bao jingine na kuisawazishia Simba, baada ya kipa wa Mbao kushindwa kudaka mpira wa Jarvie Bokungu uliomgonga miguuni na kumkuta mfungaji.

Wakati baadhi ya mashabiki wakianza kutoka uwanjani na kuridhika na matokeo ya sare ya 2-2, Mzamiru alisababisha uwanja huo wa Kirumba kujaa vumbi kwa mashabiki kushangilia kupita kiasi, baada ya shuti lake kali kutinga wavuni na kuipatia timu yake bao la ushindi na kufanya matokeo kuwa 3-2 na kuirudisha timu yake kileleni mwa msimamo.

Simba sasa ina pointi 58 wakiwazidi mahasimu wao, Yanga wenye mchezo mmoja mkononi kwa alama mbili na kuzifanya mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu kuwa na mvuto wa aina yake.

Katika mchezo huo, wenyeji Mbao FC waliwakilishwa na Erick Ngwengwe, Yusuph Ndikumana, David Mwasa, Asante Kwasi, Boniface Maganga, Vincent Philipo, George Sangija, Salmin Hoza, Pius Bushita, Ibrahim Njohole pamoja na Evaringestus Bernad.

Simba wao walikuwa Manyika Peter, Hamad Juma, Mohamed Hussein, Janvier Bokungu, Jjuuko Murshid, James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Mohamed Ibrahim, Juma Luizio pamoja na Pastory Athanas.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -