Sunday, October 25, 2020

Dakika 90 za Pochettino zilizowahi kumtoa jasho Guardiola na Barcelona yake

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England

AKIWA ndani ya dimba la White Hart Lane kama kocha mkuu wa klabu ya Tottenham Hotspurs,Mauricio Pochettino , alianza maisha yake ya ukocha katika timu ya Espanyol ya Hispania mwaka 2009.

Na ushindi wake wa kwanza aliupata dhidi ya Barcelona iliyokuwa chini ya Pep Guardiola kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Barca, Camp Nou.

Ulikuwa ni mchezo ambao wengi walitabiri Pochettino angepoteza kutokana na nafasi zao tofauti kwenye msimamo wa Ligi Kuu Hispania (La Liga). Barca ilikuwa ikiongoza, Espanyol ilikuwa ikijitutumua dhidi ya janga la kushuka daraja.

Mwaka huu, watakutana kwa mara ya kwanza England, Pochettino akiinoa Spurs na Guardiola akiwa Manchester City. Na kuelekea mpambano wao huo, SkySport umeelezea historia ya kukutana kwao kwa mara ya kwanza Hispania.

Kabla ya kukutana kwenye mchezo wa La Liga, Barcelona iliongoza msimamo kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya wapinzani wao ambapo kocha mpya, Guardiola alikuwa hajaonja uchungu wa kufungwa mbele ya mashabiki wake.

Kichapo alichokipata ndio kilikuwa cha kwanza kwake na ushindi dhidi ya Barca ndio ulikuwa wa kwanza kwa Espanyol katika kipindi cha miaka 27 ya historia ya wapinzani hao wa jadi wa jiji la Catalunya.

Barca ilikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu mno msimu huo, idadi ya mabao waliyozifunga timu mbalimbali haikupungua zaidi ya mabao manne na kuendelea.

Mwishoni mwa mwaka huo, Barca haikunyakua taji la La Liga tu bali iliyatwaa mataji ya Kombe la Mfalme (Copa del Rey), Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uefa Super Cup, Super Cup ya Hispania na Klabu Bingwa ya Dunia.

Upande mwingine wa ndugu zao, Espanyol wao walikuwa kwenye hali ngumu, wakicheza michezo 14 ya ligi bila ushindi. Ikamtimua kocha wao, Bartolome ‘Tintin’ Marquez na mrithi wake, Mane akaisaidia timu iliyokuwa kwenye pumzi yake ya mwisho.

Januari mwaka 2010, Espanyol ilianza kupata mwanga wa kusalia ligi kuu ambapo pointi tano zilianza kuwapa nguvu kabla ya Mauricio Pochettino ambaye ni beki wa zamani wa timu hiyo kukabidhiwa mikoba ya kuiokoa na janga la kushuka daraja.

Akiwa na umri wa miaka 36, Pochettino alikianza kibarua chake hicho cha kwanza kama kocha na ngao yake kuu ilikuwa ni kuimarisha nidhamu.

Tatizo kubwa lililokuwa likiisumbua sana Espanyol lilikuwa ni ukosefu wa mabao ambapo washambuliaji kama Hernan Crespo na Mario Balotelli walizungumziwa kuletwa kwa mkopo ili kuimarisha safu ya ushambuliaji lakini Pochettino aliamua kukazania mazoezi zaidi kwa wachezaji wake huku dirisha la usajili likikaribia kufunguliwa.

Mpango wake huo ulizaa matunda ndani ya kikosi, ambapo mastaa kama Ivan de la Pena na wengineo walianza kung’ara kutokana na imani waliyokuwa wakioneshwa na kocha wao huyo mpya.

Sare tatu mfululizo zilianza kurudisha hali yao ya kujiamini. Vichapo viwili vyembamba dhidi ya Barcelona kwenye Copa del Rey vilileta matumaini pia. Lakini bado walienda Camp Nou wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Sevilla wiki chache zilizopita mwaka huo. Ni matokeo ambayo kwa hali ya kawaida yasingekuwa mazuri kwao.

“Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu au wa nne tangu nianze kazi, tayari nilianza kuona mabadiliko Espanyol,” alisema Pochettino.

“Mpango wetu ulikuwa ni kucheza soka la kasi ya juu na kuwashangaza. Nakumbuka Barcelona walikuwa na Ronaldinho Gaucho, Samuel Eto’o, Thierry Henry, Yaya Toure, Eric Abidal, Carles Puyol na Andres Iniesta ambao walikuwa na kiwango cha hali ya juu na bado walishangazwa nasi.”

Pochettino alijiamini nini kutumia mfumo wa kushambulia dhidi ya Barcelona? Kwa kawaida timu ambayo ilikuwa ikikutana na wababe wa Catalunya waliokuwa na Messi, Gaucho, Xavi na Iniesta, walikuwa ni lazima ‘wapaki basi’ (walinde sana).

Lakini mfumo wake ukafanikiwa kumpa matokeo usiku wa siku. Mchezo ambao ulitajwa kama ni ‘dakika 90 za soka zilizowatisha Barca’.

Usiku huo mastaa wa Barca walihaha kusaka mabao bila mafanikio. Henry, Xavi, Lionel Messi walikosa mabao ya wazi. Seydou Keita akaoneshwa kadi nyekundu na kutoka nje. Espanyol walipoteza sana muda baada ya kupata bao, walichelewesha kila kitu uwanjani kadiri ya uwezo wao. Walicheza na soka la ‘kihuni’.

Mabao mawili ya Espanyol yalifungwa na De la Pena ambaye alikuwa ni rafiki wa zamani wa Guardiola ndani ya Barca. Toure alifunga bao moja lakini halikutosha kuiokoa Barca na kichapo.

Ulikuwa ni ushindi mtamu kwa mashabiki wa Espanyol ambao walikuwa wakilizwa na Barca kwa kipindi cha miongo mitatu (miaka 30). Kila siku walikerwa na nyimbo za mashabiki wa Barca wakiiimba timu yao kuwa inaelekea daraja la pili. Lakini siku hiyo wimbo wao ulijibiwa kwa kichapo.

Espanyol iliposhinda dhidi ya Barca, wapinzani wao Real Madrid walipata tumaini kuwa wangeweza kunyakua ubingwa wa La Liga, lakini hilo halikuwa tatizo kwa Barca kwani walinyakua pointi 25 katika michezo yao 10 ya mwisho, ushindi wa mechi nane kati ya hizo uliwafanikisha kunyakua ubingwa.

Pochettino alijitahidi kuiokoa Espanyol isishuke daraja na badaa ya muda mfupi akapata nafasi ya kutua England. Sasa akiwa Spurs, tayari ameshajizolea umaarufu akianzia Southampton.

Wikiendi hii anakutana tena na Guardiola akiwa Manchester City. Kuna uwezekano pia wa yeye kurudia alichokifanya mwaka 2009. Siku ambayo Espanyol iliishangaza Barca pale Camp Nou.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -