Tuesday, November 24, 2020

Dante aweka rekodi Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

BEKI wa kati wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’, ameweka rekodi ya aina yake ndani ya timu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kombinesheni yake kukubali kucheza na mabeki wote wa kati waliopo ndani ya kikosi hicho.

Katika dakika 360 alizocheza, beki huyo tayari amefanikiwa kutishia zama za mabeki wakongwe wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro, Kelvin Yondani na Vincent Bossou.

Safu ya mabeki wa kati wa Yanga inaundwa na mabeki wa shughuli kama Bossou, Pato Ngonyani, Cannavaro na Yondani ambao ndio amekuwa wakipata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Dante alianza rasmi kuitumikia Yanga dhidi ya Medeama akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Yondani ambaye alitoka kipindi cha kwanza baada ya kuumia nyonga kwenye mchezo huo uliopigwa nchini Ghana wa kuwania Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) hatua ya makundi.

Na kwenye mchezo dhidi ya Mo Bejaia, Dante alianza katika kikosi cha kwanza akicheza kama pacha wa beki mwingine wa timu hiyo, Bossou lakini hata hivyo hakuweza kumaliza mchezo huo baada ya kuumia dakika 15 za kipindi cha kwanza.

Tangu hapo beki huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amejihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha Hans van der Pluijm, huku akiweka rekodi ya kucheza kama pacha wa mabeki wengine wa timu hiyo, Cannavaro, Bossou na Yondani.

Dante amefanikiwa kumkuna Pluijm kiasi cha kuwafanya mabeki wengine wa timu hiyo kupokezana kucheza huku yeye akitamba kucheza katika dakika zote tisini za michezo minne ya Ligi Kuu waliyocheza mabingwa hao watetezi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -