NA KYALAA SEHEYE
WANAMUZIKI Sharifu Thabiti ‘Darasa’ na Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ wanatarajia kupimana ubavu kwa staili ya ‘nichane nikuchane’ katika Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem, kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya wa 2017.
Akizungumza na BINGWA, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo, alisema Darasa na Roma wanaimba muziki wa aina moja na wamefanikiwa kuwakamata mashabiki vilivyo, kila mmoja akijiona bora.
“Hawa wote ni wana hip hop wazuri sana, sasa tunataka wadhihirishe ukumbini nani ni mkali zaidi ya mwenzie ili kumaliza ubishi katika onyesho tulilolipa jina la Rap Battle,” alisema Mbizo.
Mbizo alisema wanamuziki hao watasindikizwa na wasanii wengine, Jahazi Modern Taarab, Msaga Sumu, H. Mbizo, Mc Darada na wengine wengi.