Saturday, November 28, 2020

DAREVA ITAFANIKIWA KURUDISHA HADHI YA VOLLEYBALL?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA GLORY MLAY

PAMOJA na mchezo wa wavu (Volleyball) kupendwa sana, lakini kwa hapa Tanzania umekosa hamasa ukilinganisha na michezo mingine  kama kikapu, soka, gofu, tenisi na masumbwi.

Miaka ya nyuma mchezo huu ulijulikana sana na kupendwa na watu,  lakini ghafla ulidorora  kutokana na  kupigwa marufuku kuchezwa shuleni jambo ambalo liliufanya kupoteza mwitikio kama ilivyokuwa awali.

Lakini sasa Chama cha Wavu Mkoa wa Dar es Salaam (DAREVA), kimejitosa kupigania kurudisha heshima ya mchezo huo nchini hasa katika shule za msingi na sekondari, ambapo mwanzoni ulikuwa umepigwa marufuku.

Mbali na chama hicho kutokuwa na fedha za kutosha kimejitahidi  kufanya juhudi mbalimbali kupitia mifuko ya viongozi  wenyewe ili kuweza kuona mchezo wa wavu unakuwa maarufu tena nchini, pia chama hicho kimefanya mambo matano kuhakikisha hadhi ya mchezo huo inarudi.

HAMASA

Dareva kupitia kwa katibu wake Yusuph Mkarambati, wamesema kuwa mchezo huu ulikosa hamasa ya kuchezwa pamoja na kufuatiliwa  kama ilivyo kwa michezo mingine kutokana na watu kutokupata mafunzo ya kutosha kuhusiana  na mchezo huo, lakini kwa  sasa watu wameanza kuhamasika na kuanza kuufutilia baada ya muda mfupi ujao utarudi tena katika hadhi iliyokuwa nayo miaka iliyopita.

Anasema mashindano na mabonanza wanayoyaandaa yanasaidia kuwavuta watu kutokana na kuwapo kwa zawadi mbalimbali kwa washiriki na mashabiki kitu ambacho kinazidi kutoa hamasa kwao na kuzidi kuupenda mchezo huo.

“Tunashukuru mpaka sasa watu wamekuwa na mwamko tofauti ilivyokuwa na awali,  hii ni kutokana na chama kuona mchezo huu unaweza kupotea hapa nchini na kuamua kuanza kuurudisha upya kwa kuandaa mashindano mbalimbali hasa ya vijana,” anasema.

Amesema kipindi cha nyuma mashabiki walikuwa hawajitokezi kwa wingi katika mashindano yoyote watakayofanya, lakini kwasasa wameanza kuhamasika na wanajitokeza kwa wingi.

MAFANIKIO

Moja ya mafanikio waliyonayo ni kutoa wachezaji wawili ambao wamesajiliwa katika timu za nje na kuzidi kuwaaminisha watu kuwa mchezo huo unalipa kama michezo mingine.

“Kama chama tunatumia kila njia kuona mchezo huu unapata mafanikio, kuna wachezaji wetu wanasajiliwa katika timu za nje ni jambo la kujivunia kuona kuwa mchezo huu unalipa na unatoa nafasi za ajira kama michezo mingine, wachezaji waliosajiliwa nje ni Jackson Mmari kwa dau la Sh milioni 13 katika timu ya Rwanda (Rwanda Energy Compay) na mwingine ni Denis ambaye ameenda Kenya.

Pia tumeweza kuandaa ligi ya vijana ambayo ilikuwa kivutio kwa watu mbalimbali waliokuwa wakitazama michezo hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa, pamoja na ligi ya mkoa itakayoshirikisha zaidi ya timu 15 za wanaume na wanawake.

“Kuandaa ligi kama hiyo halafu huna mdhamini ni mafanikio mkubwa sana katika chama, tumepiga hatua kubwa na tunataka kufanya mashindano mengi zaidi ili kuweza kuona wachezaji wetu wanasajiliwa katika timu mbalimbali za nje,” anaongeza Mkarambati.

CHANGAMOTO

Anasema suala la wadhamini limekuwa changamoto kubwa kutokana na kushindwa kutoa mchango wao pindi tunapoandaa mashindano, wamekuwa hawatoi msaada kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kwa sasa tunajisimamia wenyewe  hatuna pakwenda.

“Tumeandaa ligi ya vijana bila kutegemea mdhamini yeyote, tumekuwa tukijitegemea wenyewe bila msaada wa mtu yeyote, kampuni wala serikali, kama viongozi tunashirikiana kuona tunawezaje kujikwamua ili kufikia malengo tuliyojiwekea,” anasema Mkarambati.

Pia aliongeza kuwa changamoto nyingine ipo kwa wachezaji, wachezaji wengi hasa vijana hawana jezi, viatu na mipira na mambo mengine mengi  kama chama kinatakiwa kusimamia masuala kama hayo kutokana na vijana wengi kutoka katika familia ambazo hazina uwezo.

“Tunapounda timu ya vijana wengi wao wanakuwa hawana jezi, viatu pia usafiri wa nkuweza kuwafikisha kwenye mazoezi au mashindano kama chama tunabidi tugharamie na ukiangalia kwa sasa chama kimeelemewa na majukumu mengi na baada ya kukosa wadau wa kuunga mkono jitahada zetu,” anaongeza.

MALENGO

Kupitia mashindano mbalimbali wanayoaandaa na chama hicho, malengo ni kupata timu zitakazoshiriki michuano ya kimataifa kutokana na kukosa timu hizo kwa muda mrefu, pia kuona wachezaji wakisajiliwa katika timu za nje ili kuzidi kuleta heshima katika taifa hili kupitia mchezo huu.

“Tuna malengo mengi, nahitaji wachezaji wetu au timu zetu ziwe zinashiriki michuano ya kimataifa si kuishia kucheza hapa nchini pekee, tunataka kuona wachezaji wanazidi kusajiliwa katika timu za nje na kuweza kupata mafanikio ikiwamo kubeba medali kupitia mashindano mbalimbali.”

USHAURI

Anasema Serikali inatakiwa kupunguza au kuondoa kabisa kodi kwa vifaa vya mchezo huo, pia kusimamia sera ya kuwapo sehemu za wazi kwa ajili ya watoto kucheza na kujifundisha, lakini pia wazazi wawape watoto wao fursa ya kuendeleza vipaji vyao kwa kujifunza mchezo huo.

Mkarambati anasema vyombo vya habari na wanahabari wanatakiwa kutoegemea upande mmoja pindi wanaporipoti taarifa zinazohusu michezo na burudani, badala yake watupie jicho pia katika kuandika habari za mchezo wa mpira wa wavu ambazo zimekuwa zikipewa kisogo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -