Wednesday, October 28, 2020

DAUDI MICHAEL ‘DUMA’ Kutoka kuwa dereva taksi hadi staa wa filamu za Bongo

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA BEATRICE KAIZA

KAMA tulivyoahidi kumsaka msanii wa filamu nchini, Daudi Michel’ Duma’ ili aweze kujibu maswali yenu sambamba na kusikia ushauri wenu, Jiachie na Staa Wako imefanikisha hilo.

Tumefanikiwa kumpata msanii huyo ambaye alipata kufahamika zaidi  miongoni mwa wapenzi wa filamu na  tamthilia pale aliposhiriki tamthilia ya  ‘Siri ya Mtungi’.

Baada ya kumfikishia maswali yenu ameyajibu kama ifuatavyo:-

Swali: Sunday Beju wa Kigogo Dar es Salaam, naomba kujua historia yako Duma ulikuwa unafanya kazi gani kabla ya kuingia kwenye tasnia ya filamu?

Jibu: Nilikuwa dereva taksi pale  njiapanda ya Mabibo (Big Brother),  licha ya familia yangu kutopenda kazi yangu kutokana na kujituma mwaka 2009 nilijiunga na kundi la Bahati group na kupata mafunzo ya kuigiza kwa muda wa miezi tisa.

Baada ya hapo nilikuwa bado nafanya kazi yangu ya udereva, huku nikifikiria nifanye nini katika maisha yangu ndio nilipata jibu sahihi la kuacha kazi ya udereva na kuingia kwenye tasnia ya filamu rasmi.

Swali: Sara Tesha wa Moshi, swali langu kwa Duma, ni kweli hayati Steven Kanumba alikufa na tasnia ya filamu?

Jibu: Hapana, Kanumba hajakufa na tasnia ya filamu, lakini aliweza kufungua njia na milango ya kuifikisha mbali na kufanya itambulike nje  ya mipaka ya Tanzania, bado wasanii wapo wengi na  kazi zipo nyingi zinatoka na kufanya vizuri kila sehemu ndani na nje ya nchi.

Swali: Emmanuel Sangu wa Mpagama Iringa, ni kitu gani kinawafanya wasanii wa Bongo kuishi maisha ya maigizo kama kazi yao ambayo wanafanya?

Jibu: Kila mtu anaishi maisha ambayo anaona kwake ni sahihi, kwanini wasanii wanaishi maisha ya kuigiza ambayo wamechagua kuishi, lakini si kila msanii anaishi maisha ya kuigiza.

Swali: Peter Kasele wa Airport, mimi ni msomaji mzuri wa gazeti hili na napenda kusoma Jiachie na Staa Wako, leo naomba kujua kutoka kwa Duma, hadi sasa ni mafanikio gani ameyapata kwenye sanaa?

Jibu: Mafanikio ni mengi ambayo nimeyapata kwenye tasnia ya filamu lakini siwezi kuyataja yote nikamaliza, naweza kutaja baadhi ya vitu kama kupata nafasi ya kujulikana ndani na nje ya nchi, kufanya kazi na kampuni mbalimbali, pia nimefanikiwa kuanzisha kampuni yangu ya ‘production’ iitwayo DD Production, ukiachana na hayo namshukuru Mungu nina sehemu nzuri ya kuishi na nina usafiri.

Swali: Juma Said wa Pangani Tanga, mashabiki wako tutegemee nini kutoka kwako?

Jibu: Mashabiki wangu mtegemee kazi nzuri kutoka kwangu lakini kwa wakati huu nimewaletea filamu mpya inaitwa ‘Mchongo Sio’, ipo sokoni kwa sasa.

Swali: Naitwa Mwaku, Duma una malengo gani kwenye kazi yako ya sanaa?

Jibu: Nina malengo ya kuwa msanii mkubwa wa ndio maana najituma kwa kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa ili niweze kushika hisia za mashabiki na kutimiza malengo yangu.

Swali: Mudy Sax wa Iringa, unawapa ushauri gani wasanii wachanga ambao wanatamani kuigiza na kufikia mafanikio kama yako?

Jibu: Ni kujituma na kuwa wabunifu zaidi, kwani wasanii wamezidi kuwa wengi na kila siku wanazaliwa, pia nidhamu wawasikilize wakubwa na wadogo.

Swali: Zawadi wa Dar es Salaam, hali ya soko kwa sasa ipo vipi?

Jibu: Kwa sasa hali ya soko ni nzuri  kwani tangu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, aingie kwenye  wizara hiyo kazi za wasanii zimekuwa na ulinzi mzuri.

Wasanii wameanza kula jasho la kazi zao tofauti na miaka ya nyuma.

Ushauri: Naitwa Saumu Kishory, napenda sana tamthilia ya Siri ya Mtungi, pia napenda kutazama kazi zako, wewe ni staa wangu naomba ukaze buti ili kazi zako zizidi kutambulika kimataifa.

Jibu: Asante sana Saumu kwa kuwa shabiki wangu nakupenda na asante kwa ushauri mzuri.

Swali: Naitwa Sheka wa Mererani, ni kitu gani ambacho huwezi kukisahau katika maisha yako?

Jibu: Ni siku ambayo mama yangu mzazi alipofariki, siwezi kuisahau hii siku, Mungu amlaze mahali pema.

Swali: Sada Juma wa Magomeni, Dar es Salaam, Duma una watoto wa ngapi hadi sasa?

Jibu: Nina watoto wawili hadi sasa.

Swali: Ambokisemi Ommy wa Mkuranga, Pwani, pongezi kwa Duma kwa umahiri wake katika kuigiza, je, ni wasanii gani wa Tanzania anaowapenda na wanafanya vema katika tasnia?

Jibu: Asante kwa pongezi, wasanii ambao wanafanya vema kwenye tasnia wapo wengi sana, siwezi kuwataja wote, kifupi wale wote wanaofanya kazi nzuri ya kutoa elimu na burudani kwa jamii.

Swali: Ramadhani wa Morogoro, kazi gani ilikupa umaarufu?

Jibu: Ni tamthilia ya Siri ya Mtungi.

Swali: Naitwa Philiberth Gidion wa Runazi, Biharamulo. Duma napenda kazi yako kwani unaweza kuuvaa uhusika na kumfanya mtazamaji kuona kama kweli kumbe ni maigizo tu, je, kuna kazi yoyote ambayo umecheza na wasanii wa nje ya Tanzania na kama tayari inaitwaje?

Jibu: Nimefanikiwa kufanya tamthilia  nchini Kenya iitwayo ‘Nira’ na ni tamthilia ambayo imefanya vizuri ndani na nje ya Kenya.

Swali: Mha wa Kigoma naishi Kijitonyama, Dar es Salaam. Ni msanii gani alikuvutia hadi ukatamani na wewe kuwa msanii?

Jibu: Kuhusu mtu aliyenivutia hadi kutamani kuingia kwenye uigizaji ni marehemu Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’, wakati naingia kwenye sanaa nilitamani siku moja niwe kama wao.

Swali: Naitwa Mwalimu Selemaini wa Lindi, kazi yako ya kwanza inaitwaje na ilitoka mwaka gani?

Jibu: Kazi yangu ya kwanza nilitoa Desemba 21, 2008 iliyojulikana kwa jina la ‘Upside Down’ ambayo ilifanya vizuri na kunipa moyo wa kujituma zaidi.

Ushauri: Sadick Mgahi, mimi ni shabiki wa kazi zako, lakini kama unataka kufika mbali kwenye tasnia ya filamu unatakiwa kuacha kujikweza.

Jibu: Asante kwa ushauri mzuri.

Swali: Rukia Hassan wa Singida, Duma umeoa au bado?

Jibu: Bado sijaoa na wala sina mchumba.

Swali: Amina wa Dar es Salaam, Duma hujawahi kutamani hata siku moja kuwa msanii wa Bongo Fleva?

Jibu: Kipaji cha kuimba ninacho, mimi ni msanii mzuri wa Bongo Fleva, lakini kwa sasa nimejikita zaidi kweye filamu, muda ukifika nitatoa wimbo wangu mashabiki wangu wakae  mkao wa kula.

Hawa ni baadhi ya mashabiki wa msanii Duma ambao walijitokeza kumuuliza maswali na kumpa ushauri.

Katika toleo lijalo tunamleta kwenu mrembo, Gift Stanford’ Gigy Money’ ambaye anafanya kazi ya utangazaji na video queen katika nyimbo mbali mbali za wasanii wa Bongo Fleva.

Tumia fursa hii kumuuliza maswali na kumpa ushauri kwa kutuma sms kupitia namba iliyopo hapo juu na majibu yatapatikana katika ukurasa huu huu Jumanne ya wiki ijayo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -