Sunday, November 1, 2020

DE BRUYNE SHAKANI KUKAA BENCHI MUDA MREFU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


 

STAA wa Manchester City, Kevin De Bruyne, huenda akalazimika kukaa nje ya uwanja kwa mrefu, baada ya kukumbwa na majeraha ya goti yaliyomfanya ahudhurie hafla akiwa anatembea kwa mkongojo.

De Bruyne alionekana akiwa na wachezaji wenzake wa Man City, wakati wakihudhuria hafla ya kipindi cha makala kuhusu timu baada ya kuumia goti lake la kulia mazoezini.

Hata hivyo, Man City mpaka jana walikuwa hawajasema ni muda gani ambao Mbelgiji huyo atakaa nje ya uwanja kwa kile ambacho walikuwa wanadai ukubwa wa tatizo alilonalo nyota huyo bado halijafahamika.

“Kevin ni mchezaji mzuri na kwa bahati mbaya amekumbana na majeraha haya mazoezini, lakini bado tuna nguvu ya kutosha katika kikosi chetu,” alisema beki wa timu hiyo, Kyle Walker.

De Bruyne pia aliwahi kukosa miezi miwili katika msimu wa 2015-16, ukiwa ni wa kwanza tangu atue Man City, baada ya kupata jeraha kama hilo katika mguu huo.

Man City waliuanza msimu huu wa Ligi Kuu England kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal na huku De Bruyne akiingia kipindi cha pili, baada ya kumaliza mapumziko ya fainali za Kombe la Dunia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -