Thursday, October 22, 2020

DELE ALLI AMNUNULIA SWAHIBA WAKE BONGE LA JUMBA

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

LONDON, England

WENGI huwasahau marafiki zao pindi wanapofanikiwa kimaisha, lakini haiko hivyo kwa nyota huyo wa klabu ya Tottenham Hotspur, Dele Alli.

Imeripotiwa kuwa staa huyo wa kimataifa wa England, ametumia pauni milioni 2 (zaidi ya bilioni 5 za Kibongo) kumnunulia nyumba swahiba wake wa utotoni.

Alli, ambaye ndio kwanza ana umri wa miaka 20, alijuana na jamaa huyo, Harry Hickford, wakati walipokuwa wakisoma.

Inadaiwa kuwa wakati mama mzazi wa Alli alikuwa mlevi asiye na mfano, familia ya Hickford ilimsaidia nyota huyo, hivyo ni kama amelipa fadhila.

Gazeti la Sunday People liliwahi kuripoti kuwa baada ya mama huyo, Denise, kuhisi ingekuwa ngumu kwake kuacha pombe, aliamua kumruhusu Alli kuondoka nyumbani na kuhamia kwenye familia ya Hickford.

Mwanamama huyo ana watoto wanne na Alli aliondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 13.

Alli ambaye anaishi na mwanamitindo Ruby Mae, hivi karibuni alisitisha mawasiliano na mama yake akidai kuwa hawana uhusiano wowote.

Inaelezwa kuwa sababu kubwa ya nyota huyo kuondosha jina la Alli kwenye jezi ya Tottenham, ni uhusiano mbaya alionao na familia yake.

Itakumbukwa kuwa jezi yake anayoitumia imeandikwa ‘Delle’.

Staa huyo amedai kuwa ahisi kuwa ana uhusiano wowote na familia ya mama yake ‘cha pombe’.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -