Tuesday, October 27, 2020

DENMARK INAVYOCHANGIA MAENDELEO SEKTA YA UTAMADUNI NA SANAA BUNIFU

Must Read

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu...

NA MWANDISHI WETU


UHURU wa kujieleza, kufikisha au kueleza hisia zinazomgusa mtu juu ya jambo fulani kupitia sanaa, ni jambo muhimu katika kuhamasisha ubunifu wa mawazo na njia mbadala za kujiletea maendeleo kwa taifa lolote lile.

Hata hivyo, kwa nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania haki hii ya vijana kushiriki katika shughuli za sanaa ili kutoa hisia zao au kujiletea maendeleo haijapewa msisitizo sana ukilinganisha na sekta nyingine za kimaendeleo.

Sanaa imekuwa ikichukuliwa kama sehemu ya kiburudisho tu na kwamba anayejishughulisha nayo hana mchango mkubwa katika maendeleo na uchumi wa taifa, jambo ambalo linachangia katika kuzorota kwa sekta hii muhimu.

Kwa kulitambua hilo, Ubalozi wa Denmark kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU), ilianzisha programu ya utamaduni na maendeleo Tanzania ambayo ilizinduliwa mwaka 2015 kwa lengo la kutoa fursa kubwa kwa vijana na wanawake katika kuanzisha na kushiriki shughuli za kiutamaduni na sanaa bunifu ili kujiletea maendeleo kiuchumi.

“Uhuru wa kujieleza kupitia sanaa na utamaduni huwapa watu sauti ili kufikisha maoni yao kwa jamii. Programu hii inalenga kuwajengea uwezo vijana kupitia ushiriki wao katika shughuli za sanaa na utamaduni,” anasema Einar Jensen, Balozi wa Denmark nchini Tanzania.

“Ushiriki katika shughuli za sanaa na utamaduni pia huibua hamasa ya ubunifu na uelewa wa mambo mbalimbali ya kijamii na hivyo kuchangia katika maendeleo ya Taifa,” anaongeza Balozi Jansen.

Zaidi ya shilingi bil.2 zimetengwa ili kutekeleza mradi huo wa miaka mitatu kuanzia 2014-2017, mradi ambao Dermark  imelenga kuutumia kama  mchango wake katika juhudi za kupunguza umasikini kuleta usawa, uwajibikaji na utawala bora kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa la Tanzania kupitia shughuli za utamaduni na sanaa bunifu.

Kutokuwapo kwa takwimu za kutosha kuishawishi Serikali na taasisi za kifedha kuwekeza katika sekta ya utamaduni na sanaa bunifu, kunachangia watu wengi kuona sekta hii haina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na kuchangia katika pato la taifa, hii ndiyo sababu kubwa ya sekta hii kushindwa kukua kwa hapa Tanzania na mataifa mengine ya Afrika.

Lengo la mradi huu ni kuona vijana wakipata fursa za kushiriki kwenye shughuli za utamaduni na sanaa bunifu na kuona wanavyochangia pato katika maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa.

Malengo mengine ni kuibua na kukuza vipaji vya sanaa kwa vijana, kuimarisha uwezo wa taasisi na mashirika kwa kukuza ushirikiano baina ya wadau wa sanaa Tanzania na Afrika Mashariki.

Malengo mengine ni kusaidia katika kuboresha sera na ushauri wa kitaalamu kwa ajili ya kuwa na taarifa za kutosha juu ya utamaduni na sanaa bunifu kupitia utafiti, ukusanyaji wa taarifa na usambazaji wa maarifa.

Ofisa wa Masuala ya Utamaduni katika Ubalozi wa Denmark, Mandolin Kahindi, anasema programu hiyo inalenga kutoa fursa kwa vijana na wanawake kushiriki katika shughuli za utamaduni na sanaa bunifu ili kujiletea maendeleo hasa ikizingatiwa kuwa vijana wana mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika jamii zao.

“Programu yetu inalenga kuwajengea uwezo na kuwapa fursa vijana kupitia ushiriki wa wazi na wa kweli kwenye shughuli za utamaduni na sanaa bunifu, ikiwajumuisha wanawake na wasichana wa mijini na vijijini,” anasema Kahindi.

Ili kuweza kufikia malengo ya programu hiyo, Dermark kupitia DANIDA inashirikiana na taasisi mbalimbali zikiwemo Tamasha la Kimataifa la Filamu (Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kupitia mradi wao wa Village Panorama ambao unalenga kuonesha filamu za kuelimisha kwenye maeneo ya vijijini huko Zanzibar.

Taasisi nyingine ni Culture and Development East Africa (CDEA), ambao wanafanya utafiti juu ya namna sanaa za muziki na filamu zinavyochangia katika pato la taifa, wakati taasisi ya Soma Book Café yenyewe ikiendesha mashindano ya uandishi na usomaji wa vitabu kwa shule za sekondari nchini ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuandika, kusoma na kuchambua vitabu mbalimbali.

DANIDA tayari imeshatoa vifaa vya muziki kwenye Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za Kitanzania lengo likiwa ni kuijengea uwezo taasisi hiyo katika kutoa mafunzo yake hasa katika idara ya muziki ambayo ilikuwa na ukosefu mkubwa wa vifaa hivyo.

Programu hiyo inasaidia pia kituo cha Nafasi Arts space kujenga jukwaa na eneo la kufanyia shughuli za sanaa za maonesho, ikiwa ni njia mojawapo ya kuunganisha sanaa hizo na zile za uchoraji, uchongaji, ufinyanzi na nyinginezo ili kuamsha ari ya ushirikiano baina ya wasanii wa sanaa hizo hapa nchini na Afrika Mashariki.

“Sanaa ina uwezo mkubwa wa kuwezesha majadiliano na kupaza sauti ya umma kama haki ya msingi ya kila raia. Ni muhimu wananchi wapate nafasi ya kujieleza wenyewe kupitia sanaa, lakini pia kuibua na kukuza vipaji vyao ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi,” anasema Kahindi.

Mradi huu unaenda sambamba na utekelezaji wa malengo ya DANIDA ambayo ni kupunguza umasikini na ukosefu wa usawa na kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa huduma za kijamii, kukuza ajira na maendeleo ya kijamii, kuimarisha demokrasia na utawala bora, utawala wa sheria na kuheshimu utu wa mtu na haki za binadamu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu mbele ya Yanga, licha ya...

Kaze amuibua Zahera, aionya Simba

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema aina ya mpira unaocheza kwa sasa...

Mtibwa yaitungua Azam Jamhuri, Prisons yazidi kupeta

NA GLORY MLAY TIMU ya Azam FC imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana baada...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -