Friday, December 4, 2020

DEPAY ALIVYOFUATA NYAYO ZA ‘WACHOVU’ WATANO WA UNITED

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MANCHESTER, England


MEMPHIS Depay anavyoondoka ni tofauti na alivyokuja, huo ndio ukweli. Wakati anatua jijini Manchester akitokea PSV Eindhoven ya Uholanzi, mashabiki wengi wa klabu ya Manchester United walisema kwamba winga huyo atakuwa kama Cristiano Ronaldo ndani ya klabu yao hiyo kutokana na ubora aliotoka nao Uholanzi.

Hata hivyo, maisha ndani ya dimba la Old Trafford yaligeuka na kuwa magumu zaidi na ule wakati wa yeye kuudhihirisha ubora wake umeshamwacha, kilichobaki ni yeye kupaki mabegi na kuelekea Lyon, Ufaransa baada ya klabu hiyo kukubali ada ya uhamisho ya pauni milioni 14.7.

Alikuja kama mfungaji bora wa Eindhoven msimu wa 2014/15 kwa kufunga mabao 25 kwenye mechi 36, United ikilipa pauni milioni 25 kumsajili na kitendo cha kupewa jezi namba saba kilichochea wengi waamini kuwa Mholanzi huyo atatesa vilivyo.

Lakini ni kitu gani kimemkuta? Hata hivyo makala haya angalau yatampooza huko aendako, yeye si mchezaji pekee aliyesajiliwa kwa bei mbaya na kujikuta akishindwa kuonesha makeke yake. Hawa hapa mastaa wengine waliowahi kukumbwa na maisha kama ya Depay pale Old Trafford.

 

Juan Sebastien Veron

Ubora wa Muargentina huyu ulikuwa ni kwenye pasi. Jamaa alikuwa na uwezo wa kupenyeza ‘killer pass’ katika sehemu ngumu, yaani isiyotegemewa.

Je, uliwahi kujiuliza Sir Alex Ferguson alimsajili kiungo huyo kwa kigezo gani? Ni uwezo wake huo wa kupiga pasi murua ndio uliomshawishi Ferguson kutoa pauni milioni 28.1 mwaka 2001 na kumnyakua Veron.

Alitumika katika mechi 82 ndani ya misimu mitatu, lakini kiwango chake hakikuwa cha kuridhisha na ndipo alipouzwa kwenda Chelsea kwa ada ya pauni milioni 15 mwaka 2003, alikoichezea mechi 13 bila mafanikio na kukimbilia kwao Argentina. Kwa kilichomkuta Veron, ni dhahiri kwamba timu za England hununua wachezaji kwa gharama zisizostahili.

 

Anderson

United ilimnyakua Anderson aliyekuwa tayari na umaarufu mwaka 2007, alikuwa ni kinda la Brazil lililotabiriwa mengi. Alisajiliwa kutoka Porto ambayo ndio ilikuwa mabingwa wa ligi kuu na alitoka kunyakua kiatu cha dhahabu kwenye michuano ya Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 17 mwaka 2005.

Mwaka mmoja baada ya kutua United, Anderson aliisaidia United kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2008 dhidi ya Chelsea kwa kufunga moja ya penalti za mwisho.

Licha ya kutwaa mataji na klabu hiyo, maisha ya Anderson ndani ya United yalianza kuwa magumu. Na ugumu wenyewe ulichangiwa na uzito wa mwili na kushindwa kupambana kurudisha kiwango chake kiasi cha kuifanya United imwachie bure.

 

Wilfried Zaha

Winga huyu raia wa Ivory Coast, alinyakuliwa na United akitokea Crystal Palace alikoichezea kwenye ngazi mbalimbali za vijana mwaka 2013 kwa dau la pauni milioni 15.

Hata hivyo, kocha wa zamani wa United, Ferguson, alimrudisha tena Palace kwa mkopo lakini kwa bahati mbaya alivyorudi Old Trafford hakukutana tena na kocha aliyemsajili, alikuta utawala mpya wa David Moyes.

Hakumridhisha Moyes hata kidogo, ambapo aliishia kucheza mechi mbili tu za ligi kabla ya kurudi Palace mwaka 2015.

 

Radamel Falcao

Unaweza kuona kama United ilitumia fedha yao vizuri kwa kuilipa AS Monaco pauni milioni sita tu kumchukua Falcao kwa mkopo, lakini walipoteza fedha nyingi za bure kumlipa mshahara wa wiki ulio mkubwa ambao ni mara tatu zaidi ya fedha ya kumchukua kutoka Monaco.

Falcao alikuwa ni chui asiye na meno kwa mechi 10 za awali ambapo alifunga mabao mawili tu. Baada ya hapo alikumbwa na majeraha ya goti yaliyomweka nje ya dimba kwa miezi sita.

Aliporudi, mashabiki walitegemea makubwa kutoka kwake lakini hali iliendelea kuwa mbaya zaidi kwani aliishia kufunga mabao mawili tu na mechi 17 zilizofuatia, hakufunga tena!

 

Angel Di Maria

Maisha ya Di Maria ndani ya klabu ya United yalisikitisha mno, sababu kila aliyekuwa shabiki wake alitabiri kuuona uso wa furaha wa Muargentina huyo ndani ya dimba la Old Trafford.

Haikuwa vile walivyotabiri, hayakutokea maajabu ya uwezo wake kama ilivyokuwa pale Real Madrid, ugeni wa kuichezea Ligi Kuu England ulimtawala na kumshinda nguvu. Aliporomoka kiwango kwa kasi ya ajabu.

Alianza kulilia kurudi kwao, lakini iligundulika hiyo ilikuwa ni njia yake ya kutafuta mahala pa kutokea.

Mwisho wa siku aliipata nafasi, akaondoka United baada ya kuichezea klabu hiyo jumla ya mechi 32  na kufunga mabao manne. PSG ilimnasa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 15.7 tu. United ilikula hasara kubwa mno hapa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -