Wednesday, October 28, 2020

Depay ndiye mwenye jibu la anachokitaka, soka au usupastaa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

AMSTERDAM, Uholanzi

UJIO wake ulitawaliwa na mbwembwe za kutosha, sifa kedekede sambamba na kutabiriwa kuwa winga hatari ndani ya jezi ya Manchester United.

Yeye mwenyewe alijitabiria kufanya makubwa pale Old Trafford, akaitaka na jezi namba saba iliyokuwa ikivaliwa na mastaa kama David Beckham, Cristiano Ronaldo, Eric Cantona na George Best.

Labda hilo ndilo linaweza kuwa kosa kubwa alilolifanya, kujiingiza kwenye maisha ya presha kutaka kuvaa viatu ‘ovasaiz’.

Depay alijiamini sana kuvaa viatu vilivyomshinda hata yule winga mahiri kutoka Benfica, Real Madrid hadi United, Angel Di Maria wa thamani ya pauni milioni 59.7.

Kijana ndio alikuwa ametoka Uholanzi akiacha kumbukumbu ya moto aliouwasha ligi kuu ya nchini humo na aliamini ataenda kuuendeleza kwenye ligi iliyomshinda mmoja wa mawinga bora duniani, Di Maria.

Kuisaidia klabu ya PSV kunyakua taji la ligi kuu (Eredivisie) baada ya miaka saba kupita, pia kuchukua kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora, hizi ni sababu zilizompa nafasi Depay ya kutua United.

Mechi za mwanzo tangu United itumie pauni milioni 25 kumnyakua, Depay alionesha kiwango cha kuridhisha, akafunga mabao mawili dhidi ya Club Brugge na kuisaidia timu yake katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini kadiri kikosi cha United kilivyoanza kupoteza dira, Depay naye alianza kupotea kwenye ramani.

Akashindwa kabisa kurudia kile alichokifanya Uholanzi.

Mashabiki nao wakamgeukia kwa kumtupia lawama hasa kwenye mechi dhidi ya Newcastle, Stoke na Chelsea wakidai amewakosesha pointi za muhimu.

Nje ya uwanja anafanya kazi kubwa ya kujidhihirisha kuwa na yeye ni supastaa.

Mkongwe wa zamani wa soka la Uholanzi, Ruud Gullit, alinukuliwa akichambua maisha ya soka ya kijana mdogo Depay hasa kuhusu msimu uliopita.

“Ninachokiona kwa Memphis (Depay) ni kijana anayetaka vitu viwili kwa wakati mmoja,” alisema Gullit.

“Anataka kuwa mcheza soka mahiri na kwa wakati huo huo anataka kuwa supastaa wa dunia na vijana wamwangalie yeye tu.

“Anatakiwa kufanya hayo mambo kwa mpangilio sahihi. Anatakiwa kuonesha kiwango chake uwanjani.

“Akishapata mafanikio sasa hapo sitajali kama ataamua kuchagua maisha ya starehe au vipi, atajichagulia mwenyewe.

“Swali langu kwake ni: Unataka kuwa mtu wa aina gani utakayekumbukwa maishani? Kijana aliyependa maisha mazuri na magari yavutiayo au mwanasoka mahiri?”

Mtu ambaye atampa nafasi ya kujibu swali hilo ni kocha wa Everton, Mholanzi Ronald Koeman.

Atampa nafasi ya pekee ya kuonesha kipaji chake. Ajiamini kuwa anaweza kufanya makubwa kwenye soka gumu kama la England.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuichezea Barcelona na anayetambua namna gani ya kufanya kazi na wachezaji wenye vipaji, anatazamiwa kama ni mtu sahihi kwa Depay.

Kwa sasa anaye mchezaji mahiri mwenye kipaji, anayejituma Ross Barkley. Vipi kama Depay akiongezeka? Everton inaweza kuwa timu bora kama inavyosubiriwa na wengi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -