Friday, October 23, 2020

DEPAY: SALAH WA OLD TRAFFORD ANAYESUBIRIWA LIGI KUU ENGLAND?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England


KAMA si maisha ya starehe, huenda leo angekuwa mmoja kati ya wanasoka wanaozungumziwa zaidi barani Ulaya. Memphis Depay, winga wa kimataifa wa Uholanzi.

Wiki iliyopita, alitupia mara mbili wakati Uholanzi ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Peru iliyoshiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchini Urusi.

Kwa kufanya hivyo, Depay mwenye umri wa miaka 24 alifikia mabao matano katika mechi nane zilizopita, hivyo kuwa mshambuliaji tegemo katika kikosi hicho.

“Alimwonesha kila mmoja wetu alivyo mchezaji bora kwa sasa. Nafikiri ataendeleza moto aliouwasha. Tutaendelea kuona utamu wake katika timu ya taifa ya Uholanzi,” alisema Wesley Sneijder, ambaye ameshastaafu soka la kimataifa.

Huku Depay akiwa na furaha ya kuimiliki jezi namba 10, bado mashabiki wa kandanda ulimwenguni wanakumbuka alivyoshindwa kuitendea haki jezi namba 7 katika kikosi cha Manchester United.

Mchezaji huyo anayesifika kwa ‘bata la kufa mtu’, alinunuliwa na kocha Louis Van Gaal, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi ya mwaka 2015, huku ada ya uhamisho wake ikitajwa kuwa ni pauni milioni 25.

Kilichomsukuma Van Gaal kumchukua Depay kipindi hicho ni uwezo mkubwa aliokuwa nao mchezaji huyo akiwa katika kikosi cha Uholanzi. Kama hiyo haitoshi, Depay alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uholanzi akiwa na wababe wa soka nchini humo, PSV.

Hata hivyo, jijini Manchester mambo hayakuwa kama yalivyotarajiwa na wengi kwani mwisho wa siku hata Van Gaal aliishia kumweka benchi, ikikumbukwa zaidi kung’olewa katika kikosi kilichocheza fainali ya Kombe la FA mwaka juzi.

Kilichofuata ni staa huyo kukubali matokeo kwa kukubali kufungasha kila kilicho chake na kuondoka Old Trafford. Depay akajiunga na Olympique Lyon ya Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’.

Licha ya kukubali atimke, bado Mourinho alisema wazi kuwa Mholanzi huyo ni mmoja kati ya wachezaji anaowakubali. “Hakufanikiwa kwa miezi yake 18 lakini bado ni kijana.

“Nafikiri ni jambo muhimu kwa klabu kuendelea kukifuatilia kipaji hiki na hatuna shaka kuwa atacheza vizuri huko Olympique Lyon na hata kurejea (Man United) hapo baadaye, hakuna anayemchukia,” alisema Mourinho.

Hivi sasa, Depay ni mchezaji muhimu katika kila mchezo wa Lyon kutokana na uwezo wake wa kulisakama lango la wapinzani na msimu uliopita aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligue 1.

Tangu kutua kwake katika soka la Ufaransa, tayari ameshazifumania nyavu mara 28 na pasi zake za mwisho ‘asisti’ zimezaa mabao mengine 26.

Kwa kushirikiana na Mariano Diaz, Bertrand Traore na Nabil Fekir, wameifanya safu ya ushambuliaji ya Lyon kuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya mabeki wa timu nyingine, si tu Ligue 1 bali hata katika michuano mingine, ikiwamo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kutokana na mwenendo usioridhisha wa Man United katika siku za hivi karibuni, wachambuzi wa soka barani Ulaya wameshauri kuwa huenda si vibaya kwa Man United kumrejesha nyota wao huyo.

Ni kama walivyofanya Real Madrid ambao baada ya Cristiano Ronaldo kuwapa kisogo na kwenda kujiunga na Man United, waliamua kumgeukia nyota wao wa zamani, Mariano Diaz na kumpa jezi namba 7.

Uzuri ni kwamba, katika mkataba wa sasa wa Depay na Lyon kuna kipengele kinachowaruhusu mabosi wa Man United kumchukua kwa mara ya pili staa wao huyo.

Je, huenda Depay akawa kama Mohamed Salah ambaye misimu michache iliyopita alifeli Ligi Kuu ya England akiwa na uzi wa Chelsea, lakini sasa ni mchezaji mwenye heshima kubwa Anfield?

Hivi sasa, Salah, ambaye alifunga mabao mawili pekee kwa miaka yake miwili Chelsea, kabla ya kukimbilia Italia, ameshafunga mabao 40 licha ya kwamba ni mechi 34 pekee alizocheza (Ligi Kuu).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -