Friday, September 25, 2020

DESEMBA MOSI NA SIMBA MPYA

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NA WINFRIDA MTOI

UONGOZI wa klabu ya Simba, umeamua kufanya uamuzi mgumu kabla ya kumaliza mwaka huu 2019, kufuatia mabadiliko makubwa iliyofanya ndani na nje ya kikosi chake.

Kuanzia mwezi huu wa Desemba, Simba inatarajia kuwa katika muonekano mpya, kuanzia benchi la ufundi hadi idara nyingine kulingana na matukio yanayotokea na yanayotarajia kutokea.

Simba imekuwa katika kiwango kizuri tangu mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo ulivyokamilika na sasa wameanza vitendo.

Baada ya kuajiri Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), Senzo Mazingiza ambaye ni raia wa Afrika Kusini, mambo yameanza kupamba moto, hivyo Desemba hii, Simba inatarajia kuwa mpya kulingana na picha iliyoanza kuonekana.

Miungoni mwa mambo yanayotarajiwa kuifanya klabu hiyo ionekana mpya ni haya hapa:-

 Benchi jipya la ufundi

Tayari kocha mkuu wa kikosi cha Simba, Patrick Aussems, amethibitisha kupitia mitandai yake ya kijamii ya Twitter na Instagram kuwa amevunjiwa mkataba.

Aussems aliandika kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii jana kwamba Bodi ya Wakurugenzi Simba kupitia CEO Mazingiza, imempa taarifa yeye sio tena kocha mkuu.

Awali kocha huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii alithibitisha kusimamishwa kuitumikia Simba japo hakueleza sababu lakini DIMBA limebaini alisimamishwa kwa siku tano kutokana na kudaiwa kusafiri nje ya nchi bila ruhusa ya mabosi wake, kitendo kilichochukuliwa ni utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bodi imeweka bayana kuwa imefikia uamuzi huo baada ya Aussems kushindwa kutekeleza majukumu kwa kiwango na malengo waliyokubaliana katika mkataba wa ajira.

Taarifa hiyo ilisema, miongoni mwa malengo aliyoshindwa kuyafikia Aussems ni timu kutofika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

“Pamoja na jitihada za bodi kumpa ushirikiano Aussems baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika, bado ameendelea kusimamia timu bila kujali malengo ya kuijenga yenye ari ya mafanikio, nidhamu na ushindani katika michuano ya ndani na nje,” ilifafanua taarifa hiyo.

Kingine kilichosababisha kocha huyo kutimuliwa ni maaelezo aliyoyatoa katika kikao cha kamati ya nidhamu kilichokaa Novemba 28 mwaka huu, kuhusu tuhuma za kuondoka kituo cha kazi bila ruhusa ya uongozi wa klabu.

“Ikizingatiwa kuwa kocha alikataa kuiambia kamati ya nidhamu sehemu alipokuwa na sababu ya kwenda bila ruhusa, hata hivyo klabu imeona ni wakati muafaka kutafuta mafanikio ya kimataifa na mchakato wa kutafuta mbadala wake unaanza, kwa sasa bodi imemteua Denis Kitambi kukaimu nafasi hiyo kwa muda,” ilisema taarifa hiyo.

Tofauti na taarifa hiyo, DIMBA limepata habari za ndani kuwa kocha mpya tayari ameshapatikana, ni Mzungu pia na muda mfupi ujao ataanza kazi.

Uwanja wa mazoezi

Ndani ya wiki inayoanza kesho, Wekundu wa Msimbazi hao, wanatarajia kufanya uzinduzi wa uwanja wao wa mazoezi uliopo Bunju, jijini Dar es Salaam.

Uwanja huo wa nyasi bandia ambao umeshakamilika kwa sehemu kubwa, huenda ukaanza kutumiwa na Simba katika mazoezi kuanzia mwezi huu.

Usajili wakufa mtu

Kutokana na kutaka kusuka upya kikosi hicho na kukifanya cha ushindani, inadaiwa Simba ipo katika mawindo ya usajili wa wachezaji wakali na anayesubiriwa ni kocha huyo mpya, ili atumie kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Pamoja kusajili, kuna wachezaji wengi wanatarajia kuondoka katika kikosi hicho, wengine wakitolewa kwa mkopo kwenda timu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uzinduzi wa kadi mpya za mashabiki na wanachama

Desemba 14, mwaka huu, Simba inatarajia kufanya uzinduzi wa kadi mpya za mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Kadi hizo zinawawezesha wapenzi wa Simba kutoa michango yao kirahisi, kulipia ada na kuzitumia kuingilia uwanjani wakati wa mechi zinazohusu timu yao.

@@@@@@@@@

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -