Tuesday, November 24, 2020

Di Maria na vita ya kurejea kwenye ubora wake

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

PARIS, Ufaransa

LICHA ya kufanya vizuri msimu uliopita, mambo yameonekana kumwendea kombo staa, Angel Di Maria, pale PSG.

Ujio wa kocha mpya Mhispania, Unai Emery, umeonekana kuzima moto uliowashwa na Di Maria msimu uliopita.

Di Maria alikuwa habari nyingine alipotua PSG akitokea Manchester United.

Aliuthibitishia ulimwengu wa soka kuwa bado alikuwa na kitu kwenye miguu yake, licha ya kutupiwa virago na Louis van Gaal.

Katika msimu wake wa kwanza tu nyota huyo alifanikiwa kujenga utawala wake jijini Paris kutokana na kazi nzuri aliyokuwa akiifanya dimbani.

Uwezo wa kuzifumania nyavu, pasi za uhakika, ukokotaji mipira, mashuti makali na asisti zake zilikuwa sehemu ya ushindi wa PSG katika mbio za kutwaa ubingwa wa League 1.

Hata hivyo, msimu huu upepo mbaya umemkumba mkali huyo ambapo ameanza ligi kwa mwendo wa kusuasua.

Baada ya kushuka dimbani mara sita, pasi zake za mwisho zimezaa mabao mawili.

Pasi zote hizo alizitoa katika mchezo dhidi ya Metz. Hicho ndicho kitu pekee kizuri alichokionesha tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016-17.

Katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Caen, Muargentina huyo hakutengeneza hata bao moja, ingawa hakuonyesha kiwango kibovu kivile.

Katika mchezo dhidi ya Dijon, alipiga mashuti mawili ya mbali, hivyo ni wazi kasi yake imepungua katika shughuli hiyo.

Ni mipira mitano aliyogusa akiwa ndani ya eneo la hatari. Pia Di Maria hakufunga bao wala kutoa ‘assist’, nyota huyo hakufurukuta kwenye kiwango bora katika michezo dhidi ya Monaco na Arsenal.

Dhidi ya Monaco alicheza winga ya kushoto, ambapo ilidaiwa kuwa huenda haikuwa nafasi aliyoizoea na ndiyo maana hakucheza vizuri.

Hata hivyo, walipocheza na Arsenal, kocha Emery alimtumia Blaise Matuidi upande wa kushoto, Di Maria akapelekwa kulia, lakini nyota huyo hakuonesha uhai.

Akimzungumzia nyota huyo, mchezaji wa zamani wa Chelsea Franck alisema: “Tangu alipojiunga na PSG hafanyi kile alichokuwa akikifanya alipokuwa na Real Madrid, tangu alipokuwa Manchester United ameendelea kuporomoka.”

Wakati Zlatan Ibrahimovic alipoondoka PSG wachambuzi wengi waliamini Di Maria angeibeba timu hiyo, ingawa hata Edison Cavani alipewa nafasi.

Ni wazi kuwa huo umekuwa ni mzigo mkubwa kwa Di Maria.

Wengine wanaamini kuwa huenda kocha Emery anashindwa kumtumia staa huyo.

Wakati Laurent Blanc alipokuwa klabuni hapo, Di Maria alikuwa akitokea upande wa kulia tofauti na kocha huyo anayempanga kushoto.

Mafanikio makubwa ya Di Maria msimu uliopita yalitokana na nafasi ya upande wa kulia aliyokuwa akicheza.

Kwa nafasi hiyo ilikuwa rahisi kwake kupokea pasi na kupiga mashuti kwa mguu wake wa kushoto.

Mpaka kumalizika kwa msimu huo wa 2015-16, staa huyo alikuwa amepasia nyavu mara 10 huku pasi zake za mwisho zikizaa mabao 18.

Alikuwa na asilimia 80.5 ya pasi, lakini mpaka sasa ana asilimia 76.9.

Pia pengo la Ibrahimovic aliyetimkia Old Trafford limeonekana kutozibika kirahisi.

Itakumbukwa kuwa, Ibrahimovic alikuwa na ushirikiano mzuri na Di Maria na ndiyo walioifanya PSG itishe msimu uliopita.

Ni wazi kuwa hata Cavani ameonekana kushindwa kurithi mikoba ya straika mwenzake huyo.

Kwa sasa Di Maria hafaidiki na huduma ya Cavani kama ilivyokuwa kwa ‘Ibra’.

Ukiachilia mbali mabao manne aliyofunga dhidi ya ‘vibonde’ Caen, bado staa huyo wa zamani wa Napoli hajathibitisha ubora wake kikosini.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -