Wednesday, October 28, 2020

DIAMOND ‘ANAVYOWAAIBISHA’ KISAYANSI MASTAA WENZAKE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA JESSCA NANGAWE                 |          


 

KAMA kuna kitu wakazi wa Tandale hawatakisahau kutoka kwa staa wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond, basi ni misaada aliyowapa baadhi ya wakazi hao kama sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Oktoba 2 ya kila mwaka, Diamond husherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo mara nyingi amekuwa akijumuika na watu mbalimbali, huku akitumia siku hiyo kutoa misaada kama sehemu ya furaha yake.

Staa huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kwa zaidi ya miaka tisa sasa kupitia kazi zake, amekuwa chachu ya vijana wengi kutokana na kujipatia utajiri mkubwa kwa kipindi kifupi.

Kwa sasa staa huyo ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni 5 kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, ni habari nyingine ndani na nje ya Tanzania kwani ameweza kuteka soko la muziki wa Bongo Fleva kitaifa na kimataifa kwa asilimia kubwa na kujikuta akikubalika kila mahali kutokana na uwezo wake.

Mara nyingi msanii huyu husherehekea siku hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, lakini mwaka huu amesherehekea kitofauti zaidi kwa kulipa fadhila mtaani kwao Tandale, Dar es Salaam, baada ya kumwaga misaada mbalimbali kwa rika tofauti.

Diamond ambaye alizaliwa na kukua katika mazingira magumu, mwishoni mwa juma lililopita aligeuka gumzo sehemu mbalimbali baada ya kutoa misaada hiyo katika shughuli iliyofanyika kwenye Uwanja wa Maguniani uliopo Tandale, ambapo watu maarufu mbalimbali waliweza kuhudhuria na kumpongeza kwa moyo huo.

Mara nyingi wasanii mbalimbali wamekuwa wakitumia siku ya kuzaliwa kufanya sherehe kubwa na za kifahari huku wakitumia pesa nyingi kutimiza shughuli hiyo, huku wachache wao wakikumbuka kutoa misaada kwa jamii.

Wapo wasanii ambao hutumia kiasi kikubwa cha fedha kuhakikisha shughuli yao inafana, huku wakimwaga fedha nyingi kuonyesha ufahari ili kuhakikisha shughuli zao zinavunja rekodi na kuzua gumzo hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Tumeshuhudia sherehe za kuzaliwa za mastaa mbalimbali kama Wema, Linah, Video Vixen Lyn na wengine ambao wamekuwa wakitumia fedha nyingi kuandaa sherehe zao ambazo zimekuwa gumzo sana kwenye mitandao ya kujamii.

Licha ya msanii Diamond kufanya kufuru katika siku yake hiyo, lakini mara nyingi amekuwa akiwakumbuka watu wenye hali za chini kimaisha na safari hii ameamua kugeukia nyumbani alipozaliwa na kuamua kumwaga misaada mbalimbali.

Kitendo cha msanii huyo kutoa misaada mbalimbali, kimeonekana kupokelewa na watu kwa hisia kubwa kwani wengi wameonekana kumpongeza kwa moyo huo, huku wakitaka wasanii wengine kuiga mfano huo.

Diamond aliamua kutoa misaada kwa marika tofauti ambapo alitoa misaada kwa watoto kwa kuwafungulia bima 1,000 za afya zitakazowawezesha kupata matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja.

Msanii huyo ambaye pia ni mshindi wa tuzo za Channel O, MTV na Afrimma, pia alitoa mikopo kwa wanawake 100 ambayo itakuwa ni kati ya Sh 100,000 na 200,000 kwa kila mmoja kulingana na mahitaji yake sambamba na bodaboda 20 kwa vijana ambazo zitawawezesha kujiajiri wenyewe.

Nyota huyo ambaye ni baba wa watoto watatu, Tiffah, Nillan na Dylan, hakusahau upande wa elimu kwani amesema anatarajia kukarabati shule zote zilizopo Tandale na kuweka matanki ya maji ili yawasaidie wanafunzi kupata maji ya uhakika.

Katika hili, msanii huyu anayefuatiliwa na watu zaidi ya milioni tano katika mtandao wa kijamii wa Instagram, alisema anatarajia kwamba bodaboda hizo ambazo zote hizo zitakuwa katika uangalizi maalumu, zitatakiwa kuzalisha Sh10, 000 kila moja kwa siku na baadaye kuwezesha kununua nyingine.

Kitendo cha Diamond kinawaamsha wasanii wengine kuiga mfano na kutumia ustaa wao katika kusaidia watu wenye uhitaji kwenye jamii kwa kuwa ndiyo mambo ambayo wanapaswa kuyazingatia zaidi kama kioo cha jamii.

Hii inazidi kumpa heshima msanii huyo na kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya wengine kwa kuweza kuwasaidia katika kutatua matatizo yao na kuwavusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -