Tuesday, November 24, 2020

DIDA AWEKWA KITIMOTO YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR

HOFU ya kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam, imeifanya klabu hiyo ya Jangwani kumweka kitimoto mlinda mlango wao, Deogratius Munishi ‘Dida’, kutokana na desturi yake inayoendelea ya kufungwa mabao ya kizembe.

Kitimoto hicho kimetokana na bao la mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, alilomfunga Dida kwenye mechi ya kirafiki kati ya timu za Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Burundi, ambayo ililala kwa mabao 2-1 katikati ya wiki hii.

Pamoja na bao hilo la Stars na Burundi, pia Dida alishawahi kufungwa na Mavugo bao jingine kama hilo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba, ambao walishinda mabao 2-1, Februari 25, mwaka huu.

Jambo hilo limewafanya Yanga kushtuka mapema kabla hawajaivaa Azam kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na kocha George Lwandamina na wasaidizi wake, Juma Mwambusi, Noel Mwandila, kocha wa makipa, Juma Pondamali na Meneja wa timu, Hafidhi Saleh, juzi baada ya Dida kurejea kwenye kikosi hicho, aliwekwa chini na kuelezwa makosa yake.

Kwenye kikao hicho cha dakika 30, Pondamali alimsisitiza Dida kuwa makini golini na kumtaka kuyafanyia kazi mapema mapungufu yake kama anataka kubaki kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

“Kwanini kila mara unarudia makosa yale yale,” alihoji Pondamali.

“Usirudie makosa kama yale na kusababisha kufungwa mabao kirahisi sana,” alisema Pondamali.

Moja kati ya makosa aliyokuwa akilaumiwa kwenye kikao hicho ni kitendo chake cha kuliacha goli na kushindwa kuwakumbusha mabeki wake kuwa makini wakati wote.

“Kweli beki (Abdi Banda) alifanya kosa, lakini wewe ulishaliacha goli mapema. Lakini pia unajisahau kuwakumbusha mabeki wako kuwa makini wakati wote wa mchezo.”

“Wewe ndio unauona mchezo mzima na hata wakati mshambuliaji (Mavugo) anakuja ulimuona, ulipaswa kumpigia kelele beki wako asifanye mzaha eneo kama lile,” aliongeza Pondamali.

Mlinda mlango huyo pia alishawahi kupewa adhabu ya kusimamishwa na Azam mwaka 2013, baada ya kufungwa kizembe kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba, ambao walishinda 3-1.

Hali hiyo ya kuwekana kitimoto kwa Yanga inatokana na uhitaji mkubwa wa ushindi kwenye mechi hiyo dhidi ya Azam, ambapo kama watafanikiwa kushinda, watakaa kileleni na kusubiria vinara wa ligi hiyo kwa sasa, Simba ambao wao watacheza Jumapili hii dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Simba wanaongoza ligi hiyo, wakiwa na pointi 55, wakiwaacha wapinzani wao Yanga nyuma kwa alama mbili, huku Azam wakishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 44, kila timu ikiwa imecheza mechi 24.

Yanga wanatarajia kutumia mchezo huo wa ligi kuu kujiandaa kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria, Aprili 8 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kabla ya marudiano wiki moja baadaye.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -