Monday, November 23, 2020

DIDA, NIYONZIMA WALINDWA NA POLISI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY

KIPIGO cha mabao 2-1 ilichokipata Yanga kutoka kwa Mahasimu wao wa Jadi, Simba kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kimeibua mambo mapya na mazito kiasi cha kulifanya Jeshi la Polisi kutoa ulinzi kwa wachezaji watatu wa timu hiyo.

Kipigo hicho kinaonekana kuwachanganya Yanga ambao wameanza kumsaka mchawi, huku kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, Haji Mwinyi na Haruna Niyonzima wakinyooshewa vidole kuihujumu timu hiyo.

Baada ya mchezo huo wa juzi, Niyonzima na Dida waliondolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) kutokana na mashabiki wa timu hiyo kutaka kuwapiga.

Wanachama na mashabiki wa timu hiyo walikuwa wamewasubiri wachezaji hao katika vyumba vya kubadilishia nguo, wakiwa wamejawa hasira baada ya kukerwa  na matokeo hayo.

Hata hivyo, Niyonzima na Dida walinusurika kichapo kutoka kwa wanachama na mashabiki hao baada ya FFU kuwawekea ulinzi mkali.

“Tumewachoka lazima tuwapige tu hata popote tukapokutana nao, leo si mnalindwa sisi hatutawaacha na tutawatafuta,” walisema.

Mwinyi  ambaye ni beki wa kushoto wa timu hiyo, anashutumiwa kuwa ‘duka’ pamoja na kipa wa timu hiyo, Dida ambaye mashabiki wanasema magoli yote aliyofungwa alikuwa na uwezo wa kuyaokoa.

“Magoli yote yametokea upande wa Mwinyi, anaonekana wazi kumkaba Kichuya kwa macho, Dida naye analiacha goli makusudi kabisa, hawa tunao maana tulishasikia habari zao mapema sana,” alisema shabiki mmoja ambaye alikamatwa na Polisi kisha wakaondoka naye eneo la wachezaji na baadaye kumwachia.

Baada ya tukio hilo, BINGWA lilijaribu kuwatafuta viongozi wa Yanga kuzungumzia kadhia hiyo, lakini kila mmoja hakutaka kuizungumzia.

Jana Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa, hakupatikana kulizungumzia suala hilo, ingawa taarifa za ndani zinasema kwamba Polisi waliwaondoa wachezaji hao na kuwarejesha kwenye hoteli  ambayo timu hiyo walikuwa wameweka kambi.

Licha ya baadhi ya mashabiki na wanachama kuwanyooshea vidole baadhi ya wachezaji kama ilivyo kawaida yao, kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali naye amefunguka kuhusu makosa ya kizembe ya makipa wa timu hiyo kwenye mechi dhidi ya Simba kwa kusema hakuna na namna yoyote ya kukwepa lawama makipa hao, Dida na Alli Mustapha hasa kutokana na tabia zao na kwamba wote wametoka Simba.

Pondamali alisema alipopewa jukumu la kuwafundisha makipa wa Yanga, aliwakuta Dida, Ally Mustapha Bartheza na Juma Kaseja kutoka Simba.

“Wakati nakuja kuifundisha Yanga, nilimkuta Kaseja, Dida na Barthez; hawa wote walisajiliwa kutoka Simba sasa hapo kuna nini ukimtoa Dida, utampanga Barthez ukipata ushindi unabaki kumshukuru Mungu,” alisema Pondamali.

Pondamali alisema kuna kipindi timu ikipata ushindi unalazimika kuinua mikono na kumshukuru Mungu kutokana na mashabiki wengi wa Yanga kutokuwa na imani na makipa hao hasa katika mechi baina yao na Simba.

Baadhi ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo, walisema ufike wakati viongozi wao wachukue uamuzi mgumu kwa wachezaji ambao wanaonekana wana masilahi binafsi dhidi ya Simba.

“Mchezaji kama Niyonzima anafanya mambo ya kucheza na majukwaa wakati akijua kuwa tupo nyuma ya wenzetu na hili halijaanza leo, kwani hata katika mchezo wetu wa kimataifa wa  kwanza dhidi ya Ngaya ya Comoro, alifanya mambo kama haya, sasa ana faida gani

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -