Wednesday, January 20, 2021

DILI LA ANIFOWOSHE LIKITIKI WAMEUMIA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

download (3)NA JABIR JOHNSON

KAMA klabu ya Yanga wakifanikiwa kukamilisha usajili wa beki wa Nigeria, Issa Anifowoshe, kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza Agosti 26, mwaka huu, basi washambuliaji wa klabu zitakazoshiriki ligi hiyo watakiona cha moto.

Beki huyo ambaye jina lake kamili ni Kehinde Yissa Anifowoshe, ameonyesha kiwango kizuri kwenye majaribio anayofanya katika klabu hiyo ya Yanga na bila shaka mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita hawatakubali kumwacha kutokana na udhaifu wa safu yao ya ulinzi.

Safu ya ulinzi ya klabu ya Yanga inaundwa na mabeki kama Kelvin Yondani, Nadir Horoub ‘Cannavaro’, ambao hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na kuonekana kuwa umri umeanza kuwatupa mkono.

Hilo lilidhihirika katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United, ambapo walionekana kuzidiwa ujanja na washambuliaji, Danny Usengimana na Simbarashe Nhiri, jambo lililosababisha Cannavaro kupumzishwa kabla ya mapumziko na kuzua hofu kwa mashabiki kuhusu safu yao ya ulinzi.

Mabeki wengine ni Andrew Vicent ‘Dante’ na beki mpya wa klabu hiyo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, ambao nao hawapewi nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi hicho kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kutosha.

Presha ya mashabiki wa Yanga kuhusu timu yao kutetea ubingwa wao msimu ujao ilizidi kupanda baada ya kushuhudia kikosi cha mahasimu wao Simba wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports katika tamasha la Simba Day Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0, huku mashabiki hao wa Yanga wakiwaona kwa mara ya kwanza washambuliaji ambao wamekuwa wakiwasumbua miaka yote, Emmanuel Okwi, John Bocco ‘Adebayor’ na Shiza Kichuya, wakicheza pamoja.

Pamoja na washambuliaji hao, lakini mashabiki wa Yanga walichanganyikiwa zaidi kuona safu ya ulinzi ya Simba iliyoongozwa na nahodha wao, Method Mwanjali, akishirikiana na Salim Mbonde wakicheza mabeki wa kati, huku pembeni yao wakiwa na Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, ambaye alitoka na kumpisha Ally Shomari, baada ya kumaliza mchezo huo bila ya kuruhusu bao.

Hatimaye presha yao itakuwa imepata wa kuituliza, kwani Anifowoshe ameonekana kuwavuta wengi, huku kiwango chake kikionekana kama suluhisho la tatizo lao la safu ya ulinzi, baada ya kuondoka kwa beki wa Togo, Vincent Bossou, ambaye alikuwa tegemeo lakini walishindwana katika upande wa masilahi baada ya mkataba wake kumalizika.

Hivyo kazi ni kwa benchi la ufundi na viongozi wa klabu hiyo kumalizana na Anifowoshe, ili akipige katika kikosi hicho cha kocha George Lwandamina.

 Dakika zake 25 mazoezini

Katika dakika 25 alizofanya mazoezi kwenye kikosi hicho cha Lwandamina katika Uwanja wa Uhuru juzi jijini Dar es Salaam, alionyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kuwafanya washambuliaji wa klabu hiyo, Donald Ngoma na Amis Tambwe, waingie hofu na kumkimbia.

Baadaye alicheza na beki wa Cameroon, Fernando Bongyang na kuonyesha moto zaidi hadi Ngoma na Tambwe wakamwona nuksi kwa jinsi alivyokuwa akifanya akiwakaba kwa sifa.

“Tanzania ni nchi nzuri, Yanga nimeiona kupitia kwa meneja wangu aliyenitaka tuondoke Oman na turudi huku Afrika. Huwa najisikia furaha sana kucheza tena Afrika,” alisema beki huyo mwenye kasi na kucheza kwa mipango alipokuwa akizungumza na BINGWA.

“Yanga ina wachezaji wazuri nami najiona mwenye bahati kwani ninaweza kuendana na kasi yao, huwa nacheza beki wa kati, lakini hata kiungo mkabaji ni nafasi nyingine ninayoimudu vizuri sana,” aliongeza mchezaji huyo.

 Uchezaji wake

Anifowoshe ana urefu unaokadiriwa kufika futi sita na nchi nne, pia ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na anapiga pasi kwa wakati na zinafika kwa mhusika.

Uwezo wake wa kujipanga, kucheza mipira ya juu, kuingilia pasi za wapinzani na kuongoza wengine ni mambo ambayo yanampa nafasi kubwa ya kusajiliwa na klabu hiyo ya Yanga.

 Historia yake

Kwa mujibu wa mtandao wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Anifowoshe alizaliwa Oktoba 11, mwaka 1992 (25) jijini Lagos nchini Nigeria.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Anifowoshe alijiunga na klabu ya Al Itihad ya Omana akitokea Mountain of Fire Ministry (MFM) ya Nigeria, ambapo alipewa jezi namba 14 na kuichezea klabu hiyo hadi alipoamua kuja nchini kusaka nafasi kwenye kikosi cha Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -