Tuesday, October 27, 2020

DIMPOZ ALIPALILIA BIFU LA DIAMOND, KIBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’, amelipalilia  bifu la Nassib Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba, baada ya kusema kuwa bifu hilo lisife.

Dimpoz ameyasema hayo jana alipokuwa akihojiwa kwenye kituo kimoja cha redio ambapo alidai kuwa bifu hilo liendelee kwa sababu linaleta manufaa kwenye muziki.

“Mimi nikiulizwa hili bifu liendelee au life basi nitasema liendelee, kwani zile timu zinasababisha muziki kupiga hatua kubwa zaidi,” alisema.

Dimpoz alisema watu wabishane katika hali ya kujenga na si kuvuka mipaka na kusababisha athari.

“Mabishano yawepo watu watengeneze manufaa, kwani shabiki kwake anataka starehe na nyimbo nzuri hivyo watu wasivuke mipaka,” alisema.

Akizungumzia bifu lake na Diamond, Dimpoz alisema ugomvi wao ulianza kitambo ila ulizidi baada ya kumshirikisha Wema Sepetu kwenye wimbo wake wa Wanjara.

Alipoulizwa kama mafanikio yake kuna mchango wa Diamond alisema: “Yapo mafanikio ambayo Diamond amechangia kwangu hasa kunishawishi kutoka kwenye bendi na kuwa msanii ninayejitegemea, hivyo hata yeye kuna vitu nimechangia mafanikio yake ukianza na wimbo wa Nasema Naye kuna vipande ambavyo nilitunga mimi,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -