Friday, December 4, 2020

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi ya kuwafahamu mastaa mbalimbali.

Kenny ambaye amekuwa mwongozaji mkuu wa video za Diamond Platnumz na wasanii wengine wa ndani na nje ya WCB huku akitwa tuzo ya kimataifa ya Afrimma kutoka Marekani kama Mwongozaji Bora wa Video.

BINGWA: Kenny ni nani na uliingia vipi kwenye tasnia hii kama mwongozaji wa video?

Kenny: Nimezaliwa jijini Mbeya miaka kadhaa iliyopita nikasoma shule ya Kambarage baada ya hapo nikajiunga na chuo kusomea masuala ya umeme. Nilipomaliza nikawa napenda mambo ya video nikaja Dar es Salaam kusoma ‘online’ kuhusu video kama miezi sita hivi.

Baada ya hapo nikaanza kutafuta ‘connection’ na kama unavyojua ukishamaliza masomo lazima ufanye ‘field’ (mafunzo kwa vitendo), nikakutana na Hanscana tukatambulishana na video ya Darassa na Rich Mavoko inaitwa Kama Utanipenda ndio video yangu ya kwanza kushuhudia ikifanywa.

Kuanzia hapo nikaanza kujua, kupangilia rangi na kuhariri video na wakati huo nikawa nakutana na wasanii wengi. Harmonize ni miongoni mwa wasanii ambao tulikuwa tukikutana tunapiga stori nyingi sana, akaniambia kwanini nisiwe nafanya video zangu mwenyewe, tukakaa chini tukapanga vitu, akanitambulisha Wasafi nikaonana na Lava Lava  ambaye nilifanya naye video yangu ya kwanza inaitwa Dede.

Baada ya kufanya Dede, video ikapelekwa WCB kila mtu akaikubali, kuanzia hapo ukaribu wangu na WCB ukaanza nikawa nafanya video za wasanii wote ambao watakubaliana na mimi.

BINGWA: Kabla hujafanya video mambo gani muhimu ambayo huwa unazingatia na msanii anapaswa kuwa na vigezo gani?

Kenny: Kwanza lazima ujue ratiba, muda, ninayefanya naye kazi, wimbo wenyewe upo vipi hayo ndiyo mambo muhimu ninayozingatia. Kwa msanii awe vyovyote kiasi cha kuweza kunimudu mimi na bajeti yangu sababu mimi nafanya biashara.

BINGWA: Umeongoza video za wasanii wengi, msanii gani ni msumbufu kwa maana ya kujenga mnapokuwa ‘location’?

Kenny: Karibia wasanii wote ninaofanya nao kazi wana hiyo tabia na mimi huwa nasikiliza pia mawazo yao sababu lengo ni kutoa video kali.

BINGWA: Changamoto zipi unakutana nazo katika kazi zako?

Kenny: Changamoto kubwa ambayo nakumbana nayo ni ni muda, nipo bize sana na nyingine za kawaida.

BINGWA: Mpaka sasa umefanikiwa kupata mafanikio gani?

Kenny: Mafanikio yapo mengi, siwezi kuyataja yote ila yapo.

BINGWA: Unapitia changamoto gani unapofanya kazi na msanii mkubwa kama Diamond Platnumz?

Kenny: Kwanza kwa Diamond nimejifunza vitu vingi kupitia yeye ni mtu poa anayesapoti kijana yeyote mwenye kipaji. Ni msumbufu pale anapotaka ufanye kazi yake iwe nzuri.

BINGWA: Video gani imekupa changamoto na ipi ilikupa mafanikio?

Kenny: Video nyingi zimenipa mafanikio, kila video inaleta mafanikio yake, kuna video inaweza kukupa fedha, kuna nyingine zinaweza kukupa kujulikana na nyingine zinaweza kukupa dili. Mfano video iliyonisumbua sana ni Baba Lao lakini hiyo hiyo pia ndio ikamvutia Wizkid.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -