Monday, January 18, 2021

DIRISHA DOGO LIMEPITA, WAMEBAKIA VIKOSINI MWAO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MAREGES NYAMAKA

HATIMAYE Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara imerejea tena mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa usiku wa Desemba 15.

Katika muda wa mwezi mmoja pilika pilika za huku na kule zilichukua nafasi yake, kivutio kikubwa cha mavuno kikiwa ni kwa wachezaji waliofanya vizuri sana mzunguko wa kwanza.

Hata hivyo, kuna kundi la wachezaji lulu waliokuwa gumzo sokoni lakini wameendelea kubaki vikosini mwao licha ya majina yao kuchukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari juu ya kuzihama timu zao.

Makala hii inakuletea orodha ya wachezaji waliokuwa wakihusishwa kupata uhamisho wa kuhamia timu nyingine, miongoni mwao wakiwamo wenye madau makubwa kweli kweli, lakini hadi jana usiku saa 05:59 walijIkuta wamebakia katika viunga vyao vya zamani.

Jonas Mkude

Nahodha huyo wa Simba  kwa kiasi kikubwa alizua mvutano wa  ndani kwa ndani na viongozi akihitaji kuboroshewa maslahi yake katika mkataba ukiwamo  mshahara mnono, ambapo hatua hiyo iliyochukua siku kadhaa kabla ya kufikia maridhiano, ilitoa mwanya mkubwa kwa nyota huyo kuhusishwa na kujiunga na Yanga.

Mkude alikuwa tayari kufanya hivyo kuhamia upande wa pili kwa watani zao wa jadi Yanga, endapo klabu yake hiyo wasingefikia mwafaka alinukuliwa akisema kwamba, anahitaji kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya maisha yake.

Kiungo huyo aliyepandishwa timu ya wakubwa zaidi ya miaka mitano iliyopita akitoke timu B ya vijana, amekuwa shupavu ndani ya Simba kwa muda wote, hususani katika safu ya kiungo mkabaji ambavo hivi sasa ataungana na ingizo jipya James Kotei pamoja na mzawa mwenzake Mzamiru Yassin.

Salum Kimenya

Moja ya beki visiki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara anayekipiga Tanzania Prisons, licha ya kufukuziwa kwa udi na uvumba  na Wekundu wa Msimbazi, dau na mahitaji yake kwa ujumla lilikuwa kikwazo kwa mabosi wa Simba ambao waliongoza mbio za kumwania beki huyu.

Kimenya hadi hatua za mwisho kabisa kufungwa kwa dirisha la usajili alisimamia  msimamo wake wa timu inayomhitaji ipeleke mezani kitita cha Sh milioni 60, fedha ambayo Simba hawakuwa tayari kutoa na kumfanya beki huyo kubakia  ndani ya kikosi cha Maafande wa Jeshi la Magereza lenye maskani yake ya mkoani Mbeya.

Hassan Kabunda

Licha ya matajiri wa Bongo wenye ushawishi mkubwa wa fedha na miundombinu ya kuvutia kumshawishi mchezaji yeyote mzawa na kutoka nje ya nchi, lakini waligonga mwamba kwa kiungo huyo pamoja na uongozi wake wa timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga.

Kabunda mwenye uwezo mkubwa wa kuchezesha timu katika safu ya kiungo, ubora wake akinga’ra vilivyo mzunguko wa kwanza ukomavu wa juu mbele ya timu kubwa kama Azam yenyewe na Yanga ataendelea kuwa mwajiriwa wa Mwadui, kutokana dili lake la usajili kwenda Azam kushindwa kufanyika.

James Muhonge

Kabla ya Simba kunasa saini ya mlinda mlango Mghana, Daniel Agyei, chaguo lao la awali katika nafasi hiyo ilikuwa kwa kipa mzawa wa Stand United, James Muhonge, kutokana na umbo lake pana na aina yake ya utendaji kazi, akichagizwa zaidi kwa kuingoza vema timu yake.

Hatua ya Simba kumsajili Agyei, huku ikiwa ni timu pekee iliyoonyesha dhamira ya kuhitaji huduma ya Muhonge, kumemfanya kipa huyo awe na subira ya msimu ujao kama ikitokea ameshawishi timu nyingine kumhitaji endapo tu ataongeza jitihada za kuongeza kiwango chake zaidi ili kuwavuta wengine wamtoe kwa Wapiga debe wa Shinyanga.

Ibrahim Ajib

Licha ya kutokuwapo timu ambayo ilijitokeza wazi wazi kuhitaji huduma yake, lakini taarifa zikadai mabosi wa Yanga walikuwa tayari kumkabidhi fungu la fedha nono na mkataba wenye maslahi katika viunga hivyo vya mitaa ya Twiga na Jangwani, akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.

Ajib pia ni miongoni mwa wachezaji wachache walioitingisha Simba katika kipindi hicho cha usajili wa dirisha dogo kutokana na hitaji lake la kuboreshewa mkataba, lakini ushawishi wa Rais wa klabu, Evans Aveva, ulifanikiwa kumbakiza mshambuliaji huyo Msimbazi.

Rashid Mandawa

Mshambuliaji aliyemaliza mzunguko wa kwanza akiwa ametikisa wavu mara saba sambamba na Amissi Tambwe wa Yanga, wastani wake wa kufunga ulikuwa ni mzuri kwa nafasi yake hiyo uliwafanya Simba kumnyemelea kipindi chote cha usajili, lakini wakashindwa makubaliano ya mwisho.

Kenny Ally

Kabla ya timu ya Mbeya City kumwachia kiungo wao Joseph Mahundi aliyetimkia Azam FC, usajili wa Kenny Ally kwenda Yanga ulikuwa umeshika kasi, ingawa hadi jana moja ya viongozi wa juu wa Wanajangwani alilihakikishia BINGWA kuwa mchezaji huyo wameshindwana.

Kiungo huyo mshambuliaji atabakia kuitumikia timu yake hiyo mzunguko wa lala salama chini ya kocha Mmalawi Kinnah Phiri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -