NA CHRISTOPHER MSEKENA
DJ mkongwe nchini, Hugoline Mtambachuo ‘Dj Choka’ amesema wimbo wake mpya atakaoachia wiki hii unaoitwa, Bila Sababu alipewa na rapa Izzo Bizness kama zawadi baada ya kupona maradhi ya Kifua Kikuu.
Choka ameliambia Papaso la Burudani kuwa wimbo huo kwa mara ya kwanza ulirekodiwa na Izzo Bizness mwaka 2014 lakini haukuwahi kutoka na yeye alipoukuta studio za Uprise Music akaupenda.
“Nilipoupenda nikamcheki prodyuza Dupy, akaniambia ni wimbo wa Izzo Bizness na nilipomwomba, akasema chukua tu kaka kama zawadi ya siku yako ya kuzaliwa na kupona TB, basi nikaingiza sauti ukafanyiwa mixing upya na ninautoa wiki hii nikiwa nimemshirikisha Izzo na Godzillah,” alisema DJ Choka