LOS ANGELES, Marekani
MKALI wa mchezo wa tenisi, Novak Djokovic, amefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya ATP baada ya kumsambaratisha Gilles Muller.
Kwa ushindi wa seti 6-3 6-4, Djokovic, anayeshika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora duniani, ametinga raundi ya tatu.
Haya ni mshindano ya kwanza kwa Djokovic, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu akiuguza majeraha.
Katika mchezo mwingine, swahiba wake, Wilfried Tsonga, naye alimchakaza Albert Ramos-Vinolas kwa seti 6-3 6-4.