Thursday, October 22, 2020

DJUMA AMEKUJA SIMBA NA UBINGWA, ATAONDOKA NAO

Must Read

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

NA JONATHAN TITO


SIMBA ilikaa miaka sita bila kubeba taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara hadi ilivyofanya hivyo msimu uliopita wa 2017/2018.

Pamoja na kubadilisha makocha kutoka nchi mbalimbali, lakini hawakufanikiwa kubeba ubingwa huo wa Ligi Kuu hadi alivyotua Masoud Djuma akiwa kocha wake mkuu Pierre Lechantre.

Makocha waliopita kabla ya Lechantre na Djuma ni kama   Milovan Cirkovic wa Serbia, Patrick Liewig (Ufaransa), Abdallah Kibadeni (Tanzania), Zdravko Logarusic (Croatia), Joseph Omog (Cameroon), Moses Basena na Jackson Mayanja, wote wa Uganda.

Djuma ndiye amefanikiwa kukata kiu ya mashabiki wa klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi kwa mfumo wake wa 3-5-2 kuing’arisha Simba na kubeba taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.

Kocha huyo wa Burundi alikuja nchini kuchukua nafasi ya Mayanja na kuwa chini ya Omog, ambaye naye aliondoka na kumwacha mwenyewe kwenye timu.

Baadaye alitua Lechantre kuja kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, wakati huo Djuma ambaye ndiye alikuwa msaidizi alishaanza kuinoa timu hiyo na kushinda mechi takribani tatu.

Lakini suala la kushinda halikuwa la ajabu sana kuliko lile la kuanzisha mfumo huo wa 3-5-2 ambao mashabiki wa soka walizoea kuuona Ligi Kuu England kwenye kikosi cha Chelsea chini ya Kocha Antonio Conte na kubeba taji la ligi hiyo msimu wa 2016/2017.

Kwa upande wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mfumo huo ulikuwa mgeni, lakini Djuma aliweza kuufundisha kwa wachezaji wa kikosi hicho na Simba kuumudu na kutandaza soka safi lililokuwa likiwavutia hata mashabiki wa timu pinzani.

Kwa mara ya kwanza Djuma alianza kuutumia mfumo huo msimu uliopita dhidi ya Ndanda mjini Mtwara na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, ambayo yote yalifungwa na mshambuliaji John Bocco.

Kisha baadaye aliutumia tena dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Taifa, Djuma aliiongoza Simba kushinda mabao 4-0 mbele ya kocha wake mkuu, Lechantre, ambaye alikuwa amekaa jukwaani akiwa amekwishasaini kutumikia klabu hiyo.

Katika mchezo huo mabao yalifungwa na Shiza Kichuya, Asante Kwasi na mawili yakiwekwa kimiyani na Emmanuel Okwi, huku mashabiki wa Simba wakishuhudia soka safi.

Baadaye Djuma aliutumia tena mfumo huo mjini Bukoba dhidi ya Kagera Sugarm, ambapo alishinda kwa mabao 2-0, ambayo yalifungwa na Said Ndemla na Bocco.

Lechantre alianza kuinoa Simba katika mchezo dhidi ya Majimaji ambao walifanikiwa kushinda mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo kocha huyo alibadilisha mfumo na kutumia 4-4-2.

Pamoja na Simba kufanikiwa kushinda mchezo huo kwa mabao hayo yaliyofungwa na Bocco na Okwi, kila mmoja alifunga mawili, lakini soka la Simba kwenye mechi katika siku hiyo halikuwa la kuvutia.

Baada ya Lechantre kuona Simba wameshindwa kucheza vizuri aliamua kurudi kwenye mfumo ulioanzishwa na Djuma na kutoa dozi ya mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC na tangu hapo kocha huyo wa Ufaransa aliendelea kutumia mfumo huo hadi mwisho wa msimu.

Kuna wakati maelewano yao yalikuwa mabovu na Lechantre kuwachezesha wachezaji wenye uwezo wa kukaba kwenye eneo la kuchezesha viungo washambuliaji au wachezeshaji.

Lechantre aliwahi kumchezesha Jonas Mkude, huku kushoto na kulia kwake akiwapanga Shomari Kapombe na Kwasi badala ya wachezaji kama Ndemla, Mohamed Ibrahim, Mzamiru Yasin na Mwinyi Kazimoto, ambao katika mechi ambazo walipangwa na Djuma walionyesha kiwango kizuri.

Hali hiyo ya kutokuelewana iliendelea hadi mwishoni mwa msimu na Simba kuanza kupata ushindi wa bao moja katika kila mechi, tena kwa tabu huku soka wanalocheza likiwa si la kawaida, kuonyesha wazi kwamba Djuma hakuwa na nafasi ya kutoa ushauri wake kwenye timu.

Mwisho wa siku Lechantre aliondoka na akaletwa kocha mwingine  kutoka Ubelgiji, Patrick Aussems na kutumia mfumo mwingine tofauti na ule wa Djuma na kusababisha timu kupata sare nyingi kwenye mechi za kirafiki wakati wa maandalizi ya Ligi Kuu na mara nyingine kushinda mabao machache na kuonyesha soka la kawaida.

Tayari kuna tetesi kwamba Aussems na Djuma wametofautiana, kocha huyo mkuu akidaiwa kukataa ushauri wa msaidizi wake kwa madai kwamba hataki kufundishwa kazi.

Hali hiyo ilionekana dhahiri baada ya Djuma kuachwa jijini Dar es Salaam kwa madai amepewa kazi ya kuisoma Yanga ikicheza dhidi ya Stand United, jambo ambalo halina ukweli, kwa kuwa hiyo si kazi ya kocha msaidizi ambaye anatakiwa mechi zote awe pembeni ya bosi wake kupeana ushauri.

Umuhimu wa Djuma ulionekana dhahiri katika mechi hiyo ya Ndanda iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona baada ya kutoka sare ya 0-0 na timu ikicheza mchezo wa ovyo tofauti na msimu uliopita, ambao Djuma alikwenda na kushinda kwa mabao 2-0 na kutandaza soka safi.

Maajabu zaidi kocha Aussems ameonekana kushupaza shingo na kumwacha tena Djuma kuelekea Mwanza, ambapo leo watacheza mechi ngumu dhidi ya Mbao FC na kwa mujibu wa wa ratiba, Septemba 27, mwaka huu wanatakiwa kucheza dhidi ya Mwadui FC, siku tatu kabla ya kuvaana na Yanga.

Mchezo wa Simba dhidi ya Mbao utakuwa mgumu mno na ilipaswa Djuma kuwapo kutokana na uzoefu wake kwa timu za Ligi Kuu, lakini pia uwezo wake ni muhimu kiushauri kimbinu ili kuisaidia timu yake, lakini Aussems ameonyesha mambo ambayo hakuna sehemu nyingine yanatokea kwa kumwacha msaidizi wake.

Kama uongozi wa Simba hautakaa chini na makocha hao na kumaliza tofauti zao, wataiweka timu kwenye mazingira ya kushindwa kutetea ubingwa wao, hasa kutokana na umuhimu wa Djuma na upinzani wa ligi ya msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -