Tuesday, October 20, 2020

DJUMA ATUMA UJUMBE SIMBA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

>>Msimbazi waishukia Mbao FC na hasira kibao, Kagere aapa

>>Mbao FC wanyang’anya wachezaji simu

NA GLORY MLAY


HUKU kikosi cha Simba kikishuka katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza leo kuvaana na Mbao FC, kocha msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi hao, Masoud Djuma, ametuma ujumbe mzito kwa wapenzi wa klabu hiyo.

Kwa mara nyingine, Simba leo watacheza mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara bila Djuma ambaye pia hakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichoifuata Ndanda FC mkoani Mtwara na kuambulia suluhu mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kitendo cha Djuma kutokuwapo mjini Mtwara, kimeonekana kuwagawa watu wa Simba, baadhi wakiamini kuwa ndicho kilichochangia timu yao kutopata ushindi.

Wanaoamini hivyo wanadai kuwa Mrundi huyo ndiye anayewajulia wachezaji wake vilivyo tofauti na ilivyo kwa bosi wake, Mbelgiji Patrick Aussems.

Baada ya madai hayo, wengi walitarajia Djuma angeungana na kikosi jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa leo, lakini haijawa hivyo.

Imeelezwa kuwa Djuma amebaki Dar es Salaam ili kuendelea na programu aliyopewa na Aussems ya kuwapiga msasa wachezaji ambao hawapo katika kikosi cha kwanza, wakiwamo Haruna Niyonzima na Jjuuko Murushid.

Kutokana na hali hiyo, watu wa Simba wanajiuliza iwapo kikosi chao kinaweza kupata ushindi leo dhidi ya Mbao FC bila Djuma au la.

Bingwa lilimtafuta Djuma kuzungumzia kitendo cha yeye kubaki Dar es Salaam wakati vijana wake wakiwa ‘mzigoni’ leo Mwanza ambapo alikataa kuzungumza lolote kiasi cha kutoa ujumbe kwa wapenzi wa soka nchini kwamba kuna kitu baina yake na ama bosi wake au klabu yake hiyo kwa ujumla.

“Mimi siwezi kuzungumza lolote, nimeagizwa na bosi wangu nibaki Dar es Salaam kwa programu maalumu ninayoendelea nayo, hivyo siwezi kupinga,” alisema.

Juu ya matarajio yake kwa kikosi chao kuelekea mchezo wa leo, Djuma alisema: “Hilo muulize kocha mkuu (Aussems), yeye ndiye ana mamlaka ya kuizungumzia timu na si mimi.”

Djuma ametokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba wakiamini bila yeye hakuna jipya ndani ya kikosi chao kwa kuwa anaifahamu vizuri timu hiyo pamoja na wachezaji.

Mbali ya hilo, baadhi ya watu wa Simba wamekuwa wakivutiwa mno na ‘amsha amsha’ ya Djuma awapo uwanjani kiasi cha kuwapandisha mzuka wachezaji wake kusaka mabao pale mambo yanapokuwa magumu kwao.

Wakati huo huo, mshambuliaji hatari wa Simba, Meddie Kagere, ametamba kuuwasha moto katika mchezo wa leo kuiwezesha timu yake kutoka uwanjani na ushindi.

“Yaliyotokea katika mchezo uliopita (dhidi ya Ndanda), nimeshayasahau na akili zangu zote zipo katika mchezo wetu ujao (wa leo dhidi ya Mbao), nitafanya kila ninaloweza kuisaidia timu yangu ya Simba kupata ushindi,” alisema Kagere.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -