Saturday, October 31, 2020

DJUMA, DILUNGA WAMEREMETA BOKO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR


 

KOCHA Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, jana alijumuika na bosi wake, Patrick Aussems, katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterans, huku kiungo wao, Hassan Dilunga, aking’ara vilivyo.

Kwa takribani wiki mbili, Djuma alikuwa nje ya kikosi cha Simba kilichosafiri kwenda Mtwara kuvaana na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na hatimaye Kanda ya Ziwa, kupepetana na Mbao na Mwadui FC.

Kitendo cha Djuma kutoambatana na timu mikoani, kilizua sintofahamu miongoni mwa watu wa Simba, baadhi wakidai kuwa kingeiathiri timum, kwa kuwa Mrundi huyo ndiye aliyewazoea zaidi wachezaji kuliko bosi wake huyo, raia wa Ubelgiji.

Katika mchezo wao dhidi ya Ndanda, Simba waliambulia suluhu kabla ya kufungwa bao 1-0 na Mbao, huku wakipata ushindi wa mabao 3-1.

Matokeo hayo yalionekana kutowaridisha baadhi ya watu wa Simba, wakiamini yametokana na kitendo cha Djuma kutoambatana na timu, japo uongozi wa Wekundu wa Msimbazi hao ulipinga vikali hilo.

Habari kutoka ndani ya Simba zilidai kuwa, Djuma alibaki Dar es Salaam kutokana na maelekezo ya Aussems, kama sehemu ya mgawanyo wa majukumu, akitakiwa kuisoma Yanga katika mechi zake mbili dhidi ya Coastal Union na Singida United, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lakini pia, ilidaiwa kuwa Djuma hana maelewano na bosi wake huyo, hivyo kitendo cha kubaki Dar es Salaam, ilikuwa ni sehemu ya adhabu.

Lakini kwa mara ya kwanza, jana Djuma alijumuika na Aussems katika mazoezi yaliyofanyika Boko Veterans na kufanya kazi pamoja.

Katika mazoezi hayo, makocha hao walionekana kuwajengea zaidi stamina wachezaji wao, tayari kukinukisha Jumapili watakapovaana na watani wao wa jadi, Yanga, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya mazoezi hayo, wanachama wa Simba wanaounda Kundi (Group) la Mtandao wa Whatsapp, walimkabidi Dilunga Sh 80,000 kama mchango wao kwa wachezaji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -