Wednesday, October 28, 2020

DJUMA YAMETIMIA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU


HATIMAYE yametimia baada ya kubainika kuwa kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, muda wowote kuanzia sasa ataachana na Wekundu wa Msimbazi hao huku taarifa za ndani zikidai kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, tayari ameshatuma ‘ndoano’ kwa Mrundi huyo.

Kwa muda mrefu Djuma amekuwa hana maelewano na Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, hivyo kuhusishwa na mpango wa kuondoka Msimbazi.

Hivi karibuni BINGWA lilipenyezewa habari kuwa uongozi wa Simba ulikuwa katika mpango wa kumtema Djuma kwa madai ya kile walichokiita ‘uswahili’ unaomtofautisha na Aussems.

Katika safari za Simba kwenda Mtwara kuvaana na Ndanda, Mwanza walikoifuata Mbao FC na walipotua Shinyanga kukipiga na Mwadui, Djuma alibaki Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kocha huyo kuendelea na programu ya kuwafua wachezaji waliobaki jijini na wale wa timu B.

Lakini hatimaye makocha hao walijumuika pamoja wakati Simba ilipokuwa ikijiandaa kucheza na Yanga, pambano lililopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumapili iliyopita na timu hizo kutoka suluhu.

Na sasa imebainika kuwa muda wowote kuanzia sasa, ‘ndoa’ baina ya Simba na Djuma itafikia tamati kama alivyothibitisha kocha huyo aliyetokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Djuma alisema yupo tayari kwa lolote litakaloamuliwa na uongozi wa klabu hiyo, baada ya kikao chake cha jana jioni dhidi ya Kaimu Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’.

Taarifa za uhakika zilizolifikia BINGWA jijini jana zinasema Aussems ameusisitizia uongozi wa Simba kwamba hayuko tayari kufanya kazi na Djuma.

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Masoud alisema aliitwa na Try Again ila hakujua anaitiwa jambo gani.

Alisema anakwenda kusikiliza wito alioitiwa na bosi wake huyo huku akiweka wazi kuwa uamuzi wowote watakaoamua yupo tayari kuupokea kutoka kwa waajiri wake.

“Nimeitwa na rais, sijajua nimeitiwa nini lakini kama itakuwa suala hilo, basi nitapokea kwa mikono miwili kwani riziki yangu kwa Simba itakuwa imekwisha hapa,” alisema.

Djuma alisema kama uongozi utaamua kuendelea kubaki basi ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote hadi hapo mkataba wake utakapomalizika.

Previous articleZAHERA: OLE WAO
Next articleMBELGIJI SIMBA ATOA KALI
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -