Saturday, November 28, 2020

DONALD NGOMA ATUMBULIWA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

BAADA ya Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma, kumkashifu daktari aliyemtibu majeraha kwa kumuita ‘Dokta feki’ katika mitandao ya kijamii, daktari huyo wa zamani wa Yanga, Haroun Ali, ameamua kumtumbua mshambuliaji huyo kwa kutoboa ukweli juu ya sakata lake la kugoma kuichezea Yanga.

Haroun ameamua kufunguka akiweka kila kitu bayana baada ya Ngoma ambaye amekosa baadhi ya mechi kutokana na kusumbuliwa na majeraha, kudai kuwa hakutendewa haki na daktari huyo kutokana na kuwapa ripoti ya uongo viongozi wa Yanga juu ya tatizo linalomkabili.

“Ngoma alipaswa kusema ukweli, nimeshangazwa sana na shutuma zake za kunidhalilisha, nimemtibu na amepona lakini alitaka niandike taarifa kwamba bado anaumwa, hii ni kinyume na maadili ya kazi yangu, nilipomuuliza kwanini nifanye hivyo akasema anawadai Yanga pesa na hakuna anayemjali. Nikamwambia hilo liko nje ya uwezo wangu, nikaandika ripoti kutokana na hali halisi na alikuwa fiti kucheza,” anasisitiza Dk. Haroun.

Dk. Haroun ameliambia BINGWA kuwa yeye si daktari wa timu ya Yanga  na kwamba klabu hiyo ina daktari wake ambaye ni Samwel Bavu, lakini kutokana na uzoefu alionao katika fani ya utabibu wa michezo, amekuwa akiaminiwa na viongozi wa klabu hiyo kuwatibu wachezaji pale linapokuja tatizo sugu kwa wachezaji.

“Sijachukua hata shilingi nyekundu ya kiongozi yeyote wa Yanga, nilimtibu Ngoma kutokana na uaminifu wangu niliojijengea kati yangu na viongozi wa Yanga, sasa leo iweje anikashifu?” alihoji.

Alisema Ngoma anashindwa kuwa mkweli juu ya matatizo yake yanayomsumbua katika klabu hiyo, huku akisema mgogoro uliopo kati ya straika huyo na viongozi wake ni mishahara yake anayodai na wala si suala la kitabibu.

Haroun alisema katika ujumbe mfupi aliokuwa akitumiana na Ngoma ambao Bingwa limefanikiwa kupata nakala zake, alimweleza kamwe hatakwenda kambini kucheza mechi na Simba mpaka pale atakapolipwa stahiki zake anazodai.

“Kuna meseji hapa alikuwa anajibizana na kiongozi mmoja wa Yanga, inasema kati ya viongozi wote waliopo madarakani katika timu hiyo ya Jangwani, ni mmoja tu ambaye anamjali ambaye ni Mwenyekiti wa timu lakini wengine wote ovyo,” aliongeza Haroun.

Alisema Ngoma akiwa na akili timamu alimtumia ujumbe mfupi wa kumshukuru kutokana na kumtibia vizuri goti lake mpaka kupona na pia Mzimbabwe huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kumueleza baada ya kuumia katika mechi ya Stand United, huku akimueleza kwamba tatizo si goti tena bali ni nyonga.

“Nilimwona akishindwa kuendelea na mechi, siku ya pili nikamtumia meseji kumuuliza kama tatizo ni goti tena, akasema tatizo la sasa ni nyonga na nilimshauri awaambie viongozi wampe bajeti ya kutosha ili afanye vipimo vya uhakika, alifanya hivyo, picha za matibabu yake na ripoti ipo, niliona tatizo na nikamtibia akapona kabisa, tena ni wiki nzima kabla ya mechi na Simba,” alisema Dk. Haroun.

Alisema kwa muda mrefu straika huyo amekuwa kwenye mikwaruzano na viongozi wa Yanga, huku ishu kubwa ikiwa ni kulipwa fedha zake anazodai na kusisitiza kama ni suala la ugonjwa hivi sasa Ngoma yupo fiti.

Straika huyo aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram, ukieleza namna alivyokwazika na kile alichodai ni taarifa za uongo kutoka kwa daktari Haroun na viongozi wa Yanga kueleza uongo juu ya matibabu yake.

“Kwa muda wote huu niliokuwa kimya nimekuwa nikitukanwa, ukweli na sababu ya kutocheza kwangu ni majeraha ya goti langu. Habari nyingi zimesambaa kupitia mitandao ya kijamii zikidai sitaki kucheza eti kwa sababu nataka kuihama klabu.

“Nashangaa hizi habari zimetoka wapi!! Daktari ametumia vibaya pesa za Yanga huku akiwadanganya viongozi kuwa amekuwa akinipeleka hospitali kupata matibabu na wakati nilitibiwa hospitali nyingine tofauti.

“Baadaye aliulizwa kuhusu maendeleo ya hali yangu na akawaambia nipo tayari kucheza wakati sikuwa tayari hata kidogo. Aliwaambia tena watu wale wale kuwa jeraha langu litapona ndani ya wiki mbili wakati madaktari wataalamu wao walisema itachukua muda wa wiki 6-8.

“Huyu daktari ‘feki’ anayeitwa Haroun amesababisha kutoelewana baina yangu na timu. Hivyo, mimi na klabu tupo katika hatua ya kufanya maamuzi na muda si mrefu nitatoa taarifa rasmi za kuondoka kwangu.

Ujumbe huo umeibua hisia kali kutoka kwa Dk. Haroun na baadhi ya viongozi wa Yanga, hali iliyomfanya Dk. Haroun kuwasilisha vielelezo vyote vya matibabu ya Ngoma kwa uongozi wa Yanga na pia BINGWA kupata nakala yake ingawa alisema si vyema kuchapisha picha na mambo mengine gazetini kwa kuwa ni kinyume na maadili.

“Vielelezo vyote ni hivyo, lakini kwa waandishi lenu la msingi ni kujua jinsi Ngoma alivyokubali kwamba amepona na akaniomba nidanganye kwa kuandika kwamba bado anaumwa ili asicheze mechi, jambo ambalo nililikataa na hilo ndilo limemuuma akaamua kunichafua,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -