Sunday, January 17, 2021

DONALD NGOMA AZUA HOFU YANGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA EZEKIEL TENDWA

BAADA ya taarifa kuvuja kuwa straika wao Donald Ngoma mkataba wake unakaribia kufikia ukingoni na bado hajakaa meza moja na uongozi kufanya makubaliano mapya, hofu imetanda kwa baadhi ya mashabiki wakidhani kuwa Mzimbabwe huyo atatimka zake.

Ngoma pamoja na baadhi ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho, mikataba yao inakaribia kumalizika jambo ambalo linawaumiza vichwa baadhi ya mashabiki wakati huu timu ikikabiliwa na michuano ya kimataifa.

Taarifa za kuaminika kutoka Yanga zinadai kuwa idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni wa klabu hiyo kongwe mikataba yao imebakisha miezi sita, ambapo sheria zinawaruhusu kuanza kuzungumza na timu nyingine.

Mbali na Ngoma, taarifa hizo zinadai kuwa wachezaji wengine ambao mikataba yake imebakisha miezi michache ni Thaban Kamusoko, Amis Tambwe, Vincent Bossou pamoja na Haruna Niyonzima ambapo Obrey Chirwa pamoja na Justis Zullu, ndio wenye uhakika na maisha ndani ya kikosi hicho kwani mikataba yao haijamalizika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya mashabiki wa Yanga, walisema kuwa uongozi unatakiwa kufanya kila linalowezekana kumalizana na wachezaji hao kabla mambo hayajawa mabaya.

Huruma Anold alisema: “Kama tutawapoteza wachezaji hao akiwamo Ngoma, litakuwa ni pigo kubwa, mimi nina imani kubwa na uongozi kwamba utamalizana nao mapema iwezekanavyo.”

Kwa upande wake, Yusuph Omar alisema: “Kidogo inaleta wasiwasi kwani majina yote ya hao wanaomaliza mikataba ni wale wachezaji muhimu kwetu, ila sisi tunaamini kuwa viongozi hawawezi kuzembea juu ya suala hili la kuwapa mikataba mipya.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -