Tuesday, November 24, 2020

DORTMUND KUMKOSA REUS HADI APRILI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MUNICH, Ujerumani

TIMU ya Borussia Dortmund italazimika kuikosa huduma ya staa wake, Marco Reus, kwa muda wa siku zilizobaki mwezi huu kutokana na majeraha ya misuli ya nyama za paja yanayomkabili.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ujerumani alikumbwa na kadhia hiyo wakati wa mechi yao ya Bundesliga ambayo Dortmund walipata ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Bayer Leverkusen na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Christian Pulisic zikiwa ni dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Thomas Tuchel, alisema kuwa Reus ataikosa mechi yao ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica na baadaye uongozi wa Dortmund ukatangaza kuwa atakuwa nje hadi mwanzoni mwa mwezi ujao.

“Borussia Dortmund haitakuwa na Marco Reus kwa muda wa takribani wiki nne hadi mapema Aprili,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo iliyotumwa katika tuvuti yao.

“Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ujerumani alipata mpasuko kwenye misuli ya nyuma ya paja wakati wa mechi ya ligi ya Bundesliga dhidi ya Leverkusen na hivyo atakuwa nje ya uwanja hadi wakati wa mapumziko ya kupisha mechi za timu za taifa na vilevile ataikosa mechi dhidi ya Benfica, Hertha Berlin, Sportfreunde Lotte na Ingolstadt,”iliongeza taarifa hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -