Friday, December 4, 2020

DORTMUND v BAYERN Mechi iliyojaa visasi, ubingwa na historia kubwa Ujerumani

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DORTMUND, Ujerumani

NI LEO pale Signal Iduna Park, ambako wenyeji wa uwanja huo, Borussia Dortmund, watawakaribisha vigogo wa Bundesliga, Bayern Munich, ukiwa ni mchezo wa 28 kwa kila timu msimu huu.

Ikiwa ni mechi ya mzunguko wa pili msimu huu wa Bundelisga, utakumbukwa kuwa ile ya kwanza ilichezwa katika Uwanja wa Allianz Arena na ilikuwa Novemba 9, mwaka jana. Dortmund walitandikwa mabao 4-0.

Kuongezea hapo, katika mechi 124 kati ya timu hizo, Bayern ni kinara wa kutamba, ikiwa imeshinda mechi 58 na kupoteza 32, huku 34 zikimalizika kwa kutopatikana mshindi (sare au suluhu).

Hata hivyo, kinachoufanya mtanange wa leo uwe wa ‘kufa mtu’ na kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka la Ujerumani ni nafasi ya kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu hiyo.

Bayern Munich wamekaa kileleni wakiwa na pointi 61, wakati Dortmund wanashika nafasi ya pili kwa pengo la pointi nne tu, ambazo zitapungua na kubaki moja endapo watashinda mechi hii.

Je, Bayern watakubali kufungwa ili wapumuliwe na Dortmund kwa pointi moja? Dortmund nao watakubali kufungwa wakati wanafahamu wataongeza pengo na kufikia pointi saba?

Kingine kinachoufanya mchezo huo wa kibabe ni kasi ya timu zote mbili tangu ziliporudi baada ya mapumziko ya lazima kupisha mapambano dhidi ya janga la Corona.

Kila moja imeshinda mechi zake mbili, Bayern wakikusanya jumla ya pointi sita dhidi ya Union Berlin na Frankfurt, huku Dortmund ikitembeza vichapo kwa Schalke na Wolfsburg.

Kama hiyo haitoshi, katika mechi 20 zilizopita, Dortmund imeshinda asilimia 75 ya zile za nyumbani, wakati Bayern wao wamepoteza asilimia 15 tu wakiwa ugenini.

Linapokuja suala la safu ya ulinzi na ushambuliaji, pia kuna uhondo mwingine katika mechi hiyo. Wakati mabeki wa Dortmund wakiwa hawajaruhusu bao katika mechi tisa kati ya 20 zilizopita, Bayern wao imewatokea mara moja tu kuondoka uwanjani bila kufunga katika mechi 20 za hivi karibuni wakiwa ugenini.

DORTMUND KULIPA KISASI?

Msimu uliopita, Lucien Favre na kikosi chake cha Borussia Dortmund walikuwa moto wa kuotea mbali, lakini, walijikuta katika wakati mgumu baada ya wakali hao kushindwa kutwaa ubingwa wa Bundesliga kwa tofauti ya pointi mbili na vinara Bayern Munich.

Mbaya zaidi, wakati timu hizo zinaenda kukutana, Dortmund walikuwa vinara wa ligi hiyo, lakini walikutana na kichapo cha kuzalilisha cha mabao 5-0 na Bayern Munich kupindua meza kibabe.

Msimu huu mechi ya kwanza Dortmund alikuwa katika wakati mgumu kwa mara nyingine baada ya kufungwa mabao 4-0 na Bavarians. Je, watafanikiwa kulipa kisasi? Kwani mara zote Bayern huwa kikwazo kwa timu hiyo.

SHOO YA HAALAND, LEWANDOWSKI

Hii ni vita nyingine katika mchezo huo ambao utachezwa katika Uwanja wa Signal Iduna Park. Straika wa Bayern Munich, Robert Lewandowski atashuhudia kikosi chake cha zamani kikiongozwa na Erling Haaland kwenye safu ya ushambuliaji.

Haaland mwenye umri wa miaka 19 amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipojiunga na wakali hao wanaotumia rangi za njano na nyeusi.

Katika michezo miwili iliyopita, straika huyo raia wa Norway amefunga mabao matatu na Lewandowski kinara wa kupachika mabao ndani ya Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga amefunga mabao mawili tangu warejee mapumzikoni.

Hata hivyo, straika huyo raia wa Poland amekuwa akiziona nyavu za mabosi wake wa zamani kila anapokutana nao, kwani amefunga mabao zaidi ya 10 tangu alipojiunga na Bayern Munich misimu minne iliyopita.

MULLER, SANCHO NAO WAMO

Jadon Sancho hajafanikiwa kuanza michezo mitatu ya hivi karibuni ambayo Dortmund wamecheza, lakini winga huyo raia wa England anaongoza kwa kutoa pasi za mabao ‘asisti’ ndani ya timu hiyo. Amefanya hivyo mara 16.

Sancho anasifika kwa kasi kubwa na uwezo wa kufunga mabao, lakini eneo la utengenezaji limempa umaarufu zaidi nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 sasa.

Bayern wanajivunia kuwa na mkongwe Thomas Muller ambaye mpaka sasa ametoa asisti 17 na kuwa kinara katika orodha hiyo msimu huu ndani ya Bundesliga.

Wawili hao ni wachezaji hatari kando ya mastraika Haaland na Lewandowski, kwani hufanya kazi kubwa ya kuunganisha timu kutoka kwenye kiungo.

Wachezaji wengine wa kuchungwa upande wa Dortmund wapo akina Thorgan Hazard, Achraf Hakimi na Rafael Guerreiro, huku Bayern wakiongozwa na Serge Gnabry, Kingsley Coman na Thiago Alcantara.

Dortmund XI: Roman Burki, Manuel Akanji, Mats Hummels, Lukasz Piszczek, Achraf Hakimi, Raphael Guerreiro, Thomas Delaney, Mahmoud Dahoud, Erling Haland, Thorgan Hazard, na Julian Brandt.

Bayern Munich XI: Manuel Neuer, Benjamin Pavard, David Alaba, Jerome Boateng, Joshua Kimmich, Leon Goretzka, Thomas Muller, Ivan Perisic, Alphonso Davies, Robert Lewandowski, na Kingsley Coman.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -