Thursday, December 3, 2020

DOZI YA SERENGETI BOYS ACHANA NAYO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU, BUKOBA

TIMU ya soka ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, imeendelea kutakata katika mechi zake za kimataifa za kirafiki baada ya jana kuigaragaza timu ya vijana ya Burundi kwa kuichapa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa Serengeti Boys inayojiandaa na michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana iliyopangwa kufanyika nchini Gabon, Mei mwaka huu, ambapo imepangwa Kundi B na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola.

Serengeti Boys walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 20 kupitia kwa mchezaji wake, Mukhsin Makame, aliyemalizia mpira wa krosi iliyochongwa na Calvin Naftal.

Dakika ya 33, Kelvin Ally wa Serengeti Boys alishindwa kuongeza bao la pili baada ya kushindwa kutumia vema nafasi aliyopata na kujikuta akipiga shuti kali lililotoka nje ya uwanja.

Serengeti Boys waliendeleza mashambulizi langoni mwa Burundi na dakika ya 38, Dickson Kibabage kwa juhudi zake binafsi aliiwezesha timu hiyo kupata bao la pili.

Burundi walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao mawili yaliyowafanya kurejea uwanjani na nguvu mpya lakini wakashindwa kutamba baada ya wapinzani wao kuendeleza mashambulizi langoni mwao.

Dakika ya 62, Yohana Mkomola, alikosa bao la wazi baada ya kupiga shuti kali akiwa nje ya 18 na mpira kutoka nje, lakini dakika ya 72 aliifungia Serengeti bao la tatu kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Burundi kuunawa mpira eneo la hatari.

Serengeti Boys inatarajia kurudiana na Burundi kesho katika uwanja huo kabla ya kucheza na Ghana katika mchezo mwingine wa kirafiki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -