Friday, November 27, 2020

DSTV KUONYESHA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

WATEJA wa DStv Tanzania watakuwa miongoni mwa mamilioni ya watu duniani watakaoona mubashara tuzo za Mwanasoka Bora Afrika kupitia chaneli ya BBC Brit.

Makamu wa Rais na Meneja Mkuu wa BBC Worldwide Kanda ya Afrika, Joel Churcher, alisema tuzo hizo zitatolewa leo jioni na zitaambatana na kipindi cha dakika 15, kitakachotangazwa na mtangazaji maarufu wa ‘BBC Focus on Africa’, Peter Okwoche.

Alisema kipindi hicho kitalenga zaidi kwenye historia za wachezaji wa mpira, historia ya uzinduzi wa tuzo hizo na hatimaye kumtangaza mshindi wa mwaka huu.

Churcher alisema kwa mara ya kwanza BBC Brit wataonyesha mubashara tuzo hizo mwaka huu, kupitia DStv na kutakuwa na kipindi maalumu cha chemsha bongo kiitwacho Pointless.

“Tuna furaha kubwa kuweza kuwaonyesha mubashara watazamaji wetu barani Afrika kipindi hiki muhimu cha tuzo za wachezaji wa mpira wa miguu Afrika. Tunatazamia kutanua wigo wa utazamaji wa chaneli yetu na kuongeza watazamaji zaidi siku zijazo. Kurushwa hewani kwa tuzo hizi, kutajenga daraja la kufanikisha malengo yetu ya kuwaburudisha zaidi watazamaji wetu adhimu,” alisema.

Tuzo za BBC Mwanasoka Bora Afrika ambazo zinaendeshwa kwa zaidi ya miongo miwili sasa, itashuhudia Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane na Yaya Toure wakichuana mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -