NA ZAINAB IDDY
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia DSTV, imeanzisha burudani mpya kwa wapenzi wa soka kimataifa kwa kuzindua msimu mpya wa soka wakitumia kampeni ya ‘Tazama vyenga bila chenga’.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo, iliyofanyika jana katika ofisi zao zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kampuni hiyo, Maharage Chande, alisema mchezo wa soka unapendwa na wengi, hivyo ni vizuri kuangalia kitu halisi.
“Kuangalia na kusikiliza mpira na kuangalia na kusikiliza katika kiwango bora ni mambo mawili tofauti, hakuna asiyejua kwamba soka lina raha yake, hasa unapoangalia kinachoonekana kwa wakati.
“DSTV kwa kuwajali wateja wetu tumeamua kuwaletea kampeni ya ‘Tazama vyenga bila chenga’ ili kuwapa burudani. Huduma hii inawawezesha kuangalia soka kupitia vifurushi vyetu vyote kwa uhalisia, tena kwa matangazo ya lugha ya Kiswahili,” alisema.